Na mimi nakuunga mkono. Chama chetu ni cha "demokrasia" na "maendeleo", sasa hiyo demokrasia iko wapi ikiwa mwenyekiti kaamua kutawala peke yake? Pia hayo maendeleo yako wapi ikiwa chama hakina hata ofisi yake? Nafikiri mleta mada ana hoja ya msingi, japo wapo watakaopingana nae ili kulinda ufisadi mkubwa walioufanya ndan ya chama na wengine watapinga ili kulinda maslahi ya matumbo yao na familia zao. Wanachama tunahitaji katiba mpya itakayomuweka mwenyekiti madarakani kwa miaka kumi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano, pia katiba hiyo iwe na kipengele cha kumuwajibisha mwenyekiti na genge lake muda wowote.