Kwa Milioni 15 naweza kujenga nyumba ikakamilika na nikahamia?

Kwa Milioni 15 naweza kujenga nyumba ikakamilika na nikahamia?

Nina milioni 15 CASH na kiwanja kipo kigamboni nataka kujenga naomba kujua kwa pesa hiyo naweza kukamilisha nyumba nikahamia kabisa?
Ndio unaweza ila uwepo site maana fund maiko akiachiwa site hana huruma itatafutwa mifuko tu ya siment alafu siment yako itauzwa na wewe utapigiwa picha siment haijatosha utajikuta umetumia milion 25
 
Nina milioni 15 CASH na kiwanja kipo kigamboni nataka kujenga naomba kujua kwa pesa hiyo naweza kukamilisha nyumba nikahamia kabisa?
Nicheki Dm nikupe ramani
Inayoweza kusuit budget Yako na mahitaji yako

My WhatsApp n0756469532

Pia waweza tembelea Instagram page yangu Maramani_ujenzi
 
Nina milioni 15 CASH na kiwanja kipo kigamboni nataka kujenga naomba kujua kwa pesa hiyo naweza kukamilisha nyumba nikahamia kabisa?

Anza taratibu mkuu ,ujenzi hauhitaji mashindano ,Jitahidi upate pesa ya kujenga boma ,kuezeka na kisha kuweka grill ukimaliza hatua hiyo basi umetoboa....Jenga nyumba ya ndoto yako ila ifikie hatua ya Boma lote ,kuezeka na kuweka grill.
 
Mpigie na hesabu ya Choo, shimo la Choo pamoja na kulijengea, pesa ndogo Sana hiyo, inaweza ikatoka lakin ambayo haijapigwa plasta wala sealing board, sakafu? Kifusi, hela ya ufundi? Maji?

Hembu orodhesha kila kitu pamoja na hela ya ufundi, kupaua na Choo nione hiyo kali Sana kwa hela hiyo inatokaje pamoja na madirisha na milango
Lakini tujue hajaacha kutafuta hela wakati nyumba inajengwa zitapatikana tu za kujazilizia kufanya haya uliyoorodhesha hapa.

Kingine tuseme akishaanza ujenzi still atakuwa hana akili ya kutafuta Tsh 2mill or 3 ndani ya miezi sita ijayo kwa ajili ya kuiboresha?
 
Back
Top Bottom