Kwa milioni 18 napata gari gani nzuri?

Kwa milioni 18 napata gari gani nzuri?

Hivi, hiyo Mil 18 ndo bajeti uliyo nayo au una ka akiba hata ka Mil5 pembeni??
Kama unanunua 0km, poa. Japo hata hiyo lazima kuna vitu vidogo vya kuongezea.
Ila kama unataka hizi za mtaani, zenye plate namba za kishikaji,utalia. Bora tafuta kigali cha Mil 10, inayobaki wenga angalau Mil4 kwa ajili ya gereji.
Kwani ki Rav4 old model hakikutoshi mkuu? Unakikarabati kinakaa sawa.

Au kama vipi,jihukulie ki pikipiki BMW F800 au GS R1200. Ule maisha
 
Hapo utapata Premio first generation (2002-2007). Ukitaka 2nd generation (2008+) angalau uwe na 21mil+

Kama ni gari ya familia, una options mbili kwa bajeti hiyo. Kuna Toyota Wish (2nd generation) yenye injini ya 2ZR-FE ambayo ipo kwenye Premio 2nd generation.

Pia unaweza kuangalia Toyota Noah ya 2012 yenye injini ya 3ZR-FE. Hii ina eco mode ambayo itasaidia gari kutumia mafuta kdg kama huisukumi aggressively. Usiende kwenye Noah zenye injini za 3S au 1AZ.
Hivi hizo Toyota wish mnazipendea nini gari imejaa kama Boti
 
1. Ukilinganisha Probox ya 2018, na Voltz ya 2004, Voltz ina ushuru mkubwa kuliko Probox.

2. Probox ya 2010 ina ushuru mkubwa (7.6mil), huku Probox ya 2018 ina ushuru mdogo (7.3mil).
Nchi ngumu sana hii Yani gari inatofauti ya umri Kwa miaka 8 ila tofauti ha Kodi ni laki 3 tu
 
Mkuu hii reply yako huwa inanifikirisha sana.
Ulikuwa mtu wa nondo za moto...sijui umekumbwa na nini!
Historia yako na yule manzi (wa hapa jukwaani) sijui inachangia hali hii!?
Yote kwa yote maisha ni kuchagua...pole mkuu.
Huyo aliendekeza mapenzi ameshakuwa chizi kapigwa na kitu kizito
 
Back
Top Bottom