UTT ni stress free with very minimal risk. Hii ndio ningemshauri afanye. Yaani unaweka mzigo wa 30m, una uhakika wa zaidi ya 99% kuvuna kiasi kisichopungua 250k kila mwezi, immediately throughout the life! Uzuri wa UTT, thamani ya pesa yako inalindwa, unaweza kutumia kama dhamana ya kukopokea benki, na utamu zaidi wakati wowote (ndani ya wiki mbili) unaweza kuzichukua pesa zake zote ulizowekeza ikiwa utabadili mtazamo.
Kuhusu kujenga nyumba ya biashara, hiyo kitu inahitaji mambo kadhaa, kwa mfano:
1. Upate kiwanja. (Wapi? Bei?), ukikosea hapo, pesa inateketea na biashara haiwezi kufanyika.
2. Ramani bora. (Sio kila nyumba inaweza kufaa kupangisha popote)
3. Ujenzi (Gharama za ujenzi haziko constant)
4. Uimara wa nyumba (itadumu katika ubora wake kwa muda gani?)
5. Ukarabati (Haijarishi ni nyumba ya namna gani, kuna ukarabati ni muhimu/lazima ufanyike ndani ya miaka mitano mitano ambao utagharamu up to 10% ya thamani ya nyumba yenyewe.
6. Kupata wateja wa uhakika. (Kujenga nyumba ni jambo moja, kupata wateja wa uhakika kwa wakati wote hilo ni jambo lingine tofauti)
7. Usumbufu wa wapangaji (Hili ndio balaa kubwa, mwanzoni wanaweza kuonyesha uungwana, lakini muda unavyozidi kusogea utaona kila rangi).
Ushuhuda.
Kuna mtu kajenga nyumba nzuri ya kupangisha maeneo ya mbeya mjini, ina apartment tatu (kila moja ni Chumba, sebule, choo na jiko) kwa milioni 70, anapangisha kila moja kwa 80k kwa mwezi (jumla ya 240k kila mwezi), kuna wakati inaweza kukaa miezi hadi minne mpaka sita bila kujaa wapangaji, na kila akitoka mpangaji mmoja anafanya ukarabati wa wastani wa laki mbili.