Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Wastani wa gawio kwa miaka 5/10 nyuma upoje? Maana hii assumption uliyoweka factor lazima ibase katika miaka 5/10 iliyopita ndo "with other factors remain constant" unaweza kuassume kuwa utapokea same rate kwa 5 years mbeleni.Hii hapa ndani ya miaka mitano nitakuwa na faida ya milion 22. View attachment 2884292
Halafu ukumbuke sisemi kuwekeza katika vipande vya hisa si sawa, nasema sio option ambayo binafsi ningeichukua sababu naamini katika biashara ya real estate na naifanya.
Faida naweza peleka huko ila si mtaji. M 30 nikitulia vizuri napata eneo zuri nje ya mji linalokuwa kwa kasi jirani na maeneo ambayo yana majina.
Nilitoa mfano kerege ni pwani ila ni jirani na mbweni na linakua kwa kasi, nanunua, nazungusha fensi ya wiremesh, naweka geti la kawaida navuta maji au nachimba kisima kama itawezekana isipowezekana naacha, naweka kibanda cha mbao na kachoo simple, nampa mtu akae bure atunze mazingira kisha natulia nikisubiri simu za madalali. Kama eneo ni zuri na watu wanajenga kwa kasi in 3 years naweza pata karibu mara mbili hata na zaidi ya nilichowekaza. Nina uzoefu.
Hapo sina mawazo kuwa bidhaa itaoza, hisa zitaanguka, sijui serikali imekopa fedha za UTT haijarudisha. Ila huyo ni mimi, wewe una mtazamo tofauti na upo sahihi.