Kwa Milioni 30, UTT amis na nyumba ya kupangisha kipi bora?

Hii hapa ndani ya miaka mitano nitakuwa na faida ya milion 22. View attachment 2884292
Wastani wa gawio kwa miaka 5/10 nyuma upoje? Maana hii assumption uliyoweka factor lazima ibase katika miaka 5/10 iliyopita ndo "with other factors remain constant" unaweza kuassume kuwa utapokea same rate kwa 5 years mbeleni.

Halafu ukumbuke sisemi kuwekeza katika vipande vya hisa si sawa, nasema sio option ambayo binafsi ningeichukua sababu naamini katika biashara ya real estate na naifanya.

Faida naweza peleka huko ila si mtaji. M 30 nikitulia vizuri napata eneo zuri nje ya mji linalokuwa kwa kasi jirani na maeneo ambayo yana majina.

Nilitoa mfano kerege ni pwani ila ni jirani na mbweni na linakua kwa kasi, nanunua, nazungusha fensi ya wiremesh, naweka geti la kawaida navuta maji au nachimba kisima kama itawezekana isipowezekana naacha, naweka kibanda cha mbao na kachoo simple, nampa mtu akae bure atunze mazingira kisha natulia nikisubiri simu za madalali. Kama eneo ni zuri na watu wanajenga kwa kasi in 3 years naweza pata karibu mara mbili hata na zaidi ya nilichowekaza. Nina uzoefu.

Hapo sina mawazo kuwa bidhaa itaoza, hisa zitaanguka, sijui serikali imekopa fedha za UTT haijarudisha. Ila huyo ni mimi, wewe una mtazamo tofauti na upo sahihi.
 
Kama unaweza kununua ardhi/shamba ambalo kuna TP au urasimishaji wa jumla na muuzaji jina lake lipo kwenye zoezi hilo la urasimishaji, basi nunua.
Pima (survey) na miliki viwanja hivyo ukiwa na hatimiliki ya wizara ya ardhi.
Halafu subiri.
 
Wazo zuri.
 
Ni kerege ipi karibu na mbweni utapata kiwanja cha milion 30 na ndani ya hiyo milion 30 uzungushie Hicho kiwanja, uweke Banda la mlinzi , uvure maji. N.k halafu ndani ya miaka miwili uuze milion 60.

Hayo maeneo hapo kerege nayajua tangu mwaka 2021 hayajapata wateja Tena Kwa milion 19. Kama uko tayari sema NIKUPE namba za mmiliki ni mbibi anaishi huko huko na ni eneo liko poa.

Halafu nani kakwambia UTT AMIS Huwa hawalipi!
 
Asubiri means that anatakiwa kuwa na kipato kingine Cha Pembeni.
 
Hongera sana Mkuu, Jenga Guest, usijenge nyumba ya wapangaji. Wapangaji wana usumbufu mwingi sana.
 
Ni kerege ipi karibu na mbweni utapata kiwanja cha milion 30 na ndani ya hiyo milion 30 uzungushie Hicho kiwanja, uweke Banda la mlinzi , uvure maji. N.k halafu ndani ya miaka miwili uuze milion 60.
Mm sijasema nitafanya haya yote kwa 30M, nimesema nitatumia hiyo 30m kupata plot.
Hayo maeneo hapo kerege nayajua tangu mwaka 2021 hayajapata wateja Tena Kwa milion 19. Kama uko tayari sema NIKUPE namba za mmiliki ni mbibi anaishi huko huko na ni eneo liko poa.
Ninayajua hayo maeneo yote huna haja ya kunipa connection boss.
Halafu nani kakwambia UTT AMIS Huwa hawalipi!
Nani kasema huwa hawalipi?
 
Tunaweza kutofautiana kimtazamo lakini ukweli unabakia pale pale, kwa Tanzania yetu hii, ukiondoa uwekezaji kama wa UTT, karibu biashara zingine zote ni pasua kichwa. Usipoibiwa na watu, utafirisiwa na Serikali. Utitiri wa makodi, matozo na blah blah kibao.
 
Hauhitaji uwe na Akili kubwa, ujanja, uchakarikaji au usimamizi wowote ili uwekeze kwenye UTT na uvune faida. Ni suala la kuamua tu. Unaweka mzigo wa 30m leo, baada ya hapo unalala usingizi wa fofo huku kila mwezi unakunja zaidi ya 250k bila blah blah. Ukichoka unakwenda kuwaambia wakupe mkwanja wako, ndani ya siku chache mzigo wako upo mfukoni. It is simple and easy.
 
Naam mkuu,pesa inaingia ukiwa umelala. Uzuri kuna compound interest,,means hyo faida unaweza kuiacha bila kuchukua. Unaendelea kuwekeza. Mwanzo wa mwaka faida inajumuishwa na mtaji na inaanza ku roll upya
 
Kwenye nyumba hapo kwa m30 inawezekana changamoto ni kiwanja kiwe sehemu nzuri na mji uliochangamka ambapo kupangisha ni big deal kama Dar, Dom , Mwanza or Arusha kama sehemu sio nzuri kwa kweli ni mtihani, hutakosa kabisa wapangaji ila return itakuwa ndogo sana

Vyumba za kupangisha siku hizi nyingi ni apartment mf. Master na Sebule, master peke yake, master sebule jiko etc kutegemea na aina ya wapangaji unaowatarget, so unaweza kuwa na ramani ya apartment hata unit nne ukajenga boma lote na kuezeka kisha ukafanyia finishing apartment moja or 2 nyingine unajikusanya mdogo mdogo maana nyumba huwa ina desturi ya kujijenga ikianza kuingiza hela
 
Leta picha/mfano halisi. Hicho ulioongea ni sawa na siasa ya ccm kusema nipeni kula nitawapa maendeleo, mwisho eake ni mgawo wa umeme na vilio lukuki.
 
Hapa bishara ya kupangisha ninapo hiona ni kichaa . Yani 70m unapata kila mwezi 240k, kwa mwaka 2,880,000 . Ni ujinga huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…