Kwa milioni 5 naweza kujenga nyumba ndogo Dodoma?

Kwa milioni 5 naweza kujenga nyumba ndogo Dodoma?

Bei ya kiwanja kisasa n nzuri sanaa kwann usifanye kujiongeza hiyo million tano tafuta kiwanja hata ihumwa au nala bei nafuu sana hata 1M unapata kizur afu cha kisasa unauza unajenga nyumba yako nzur kabisa n mtazamo tu
 
Bei ya kiwanja kisasa n nzur sanaa kwann usifanye kujiongeza hiyo million tano tafuta kiwanja hata ihumwa au nala bei nafuu sana hata 1M unapata kizur afu cha kisasa unauza unajenga nyumba yako nzur kabisa n mtazamo tu
Ushauri mzuri ila kuna watu wanapenda kuishi sehemu zenye majina makubwa kuna jamaa mji fulani ivi kajenga kajumba ka ajabu kweli hata 1m haifiki but kiwanja kipo sehemu nzuri sana akipauza hakosi 30m to 40m hapo atapata mtaji na nyumba kubwa tu lakin hataki kuuza watu wanamjia lakin wapi
 
Unajenga na ela inabaki.
simkatishi tamaa, ujenzi ni kwenda nao taratibu kadri unavyopata pesa.

Nina kibanda cha chumba 1, subule, choo na veranda ya mbele.
Nilikuwa na 2.5M kwa ajili ya finishing ( kuflush kuta na gypsum, kuweka gypsum board, rangi ndani na tiles,)
huwezi amini pesa haikutosha hapo wirering, plaster, septic tank vilikuwa tayari. Plan ilikuwa nihamie, imeshindikana....

Mtaani waliniaminisha kuwa nikiwa 6-7M ningehamia, hapa ishakula zaidi 10M
najaribu kuainisha vitu nilivyonunua na kulipia.
Nyumba ina 27 meter square
1. Box 18 tiles 40x40 pocyline @ 35,000 = 630,000
2. Box 2 tiles 40x40 pocyline black @52,000 = 104,000
3. box 13 tiles 20x40 ceramic ukuta choon @17,000=221,000
4. box 2 tiles 30x30 chooni chini @ 19,000 = 38,000
5. Scatting pc 60 @ 2,000 = 120,000
6. Cement mifuko 9 @ 15,500 = 139,500
7. Mchanga lain lori 1 (4M3) = 150,000
8. Gypsum powder mifuko 6 @ 22,000= 132,000
9. white cement mifuko 4 @ 31,000 = 124,000
10. Gypsum board 10 @ 19,000= 190,000
11. Mikanda 18 @ 3,000= 54,000
12.Rangi silk 20 lts 160,000
13.Rangi ya maji 20 lts 29,000
14. Puti 40kg 35,000
15. vioo vya milango 4, madirisha 2 = 275,000

Choo
Sink la choo =18,000
pvc 2 class B @ 30,000= 60,000
mixer za bomba 108,000

Fundi tiles ndani 5000 x 27msq = 135,000
Chooni 5000 x17 msq =85,000
Fundi bomba 85,000
Fundi rangi pamoja na kuweka vioo 180,000

Jumla = 2,964,500
 
Back
Top Bottom