simkatishi tamaa, ujenzi ni kwenda nao taratibu kadri unavyopata pesa.
Nina kibanda cha chumba 1, subule, choo na veranda ya mbele.
Nilikuwa na 2.5M kwa ajili ya finishing ( kuflush kuta na gypsum, kuweka gypsum board, rangi ndani na tiles,)
huwezi amini pesa haikutosha hapo wirering, plaster, septic tank vilikuwa tayari. Plan ilikuwa nihamie, imeshindikana....
Mtaani waliniaminisha kuwa nikiwa 6-7M ningehamia, hapa ishakula zaidi 10M
najaribu kuainisha vitu nilivyonunua na kulipia.
Nyumba ina 27 meter square
1. Box 18 tiles 40x40 pocyline @ 35,000 = 630,000
2. Box 2 tiles 40x40 pocyline black @52,000 = 104,000
3. box 13 tiles 20x40 ceramic ukuta choon @17,000=221,000
4. box 2 tiles 30x30 chooni chini @ 19,000 = 38,000
5. Scatting pc 60 @ 2,000 = 120,000
6. Cement mifuko 9 @ 15,500 = 139,500
7. Mchanga lain lori 1 (4M3) = 150,000
8. Gypsum powder mifuko 6 @ 22,000= 132,000
9. white cement mifuko 4 @ 31,000 = 124,000
10. Gypsum board 10 @ 19,000= 190,000
11. Mikanda 18 @ 3,000= 54,000
12.Rangi silk 20 lts 160,000
13.Rangi ya maji 20 lts 29,000
14. Puti 40kg 35,000
15. vioo vya milango 4, madirisha 2 = 275,000
Choo
Sink la choo =18,000
pvc 2 class B @ 30,000= 60,000
mixer za bomba 108,000
Fundi tiles ndani 5000 x 27msq = 135,000
Chooni 5000 x17 msq =85,000
Fundi bomba 85,000
Fundi rangi pamoja na kuweka vioo 180,000
Jumla = 2,964,500