Kwa milioni 5 naweza kujenga nyumba ndogo Dodoma?

Mkuu garama za ujenzi pamoja na vifaa vya ujenzi dodoma vmepanda sana, kutokana na serikali kuhamia, M 5 Kwa Dodoma hiyo inatosha kununua kiwanja tu, labda kama kiwanja unacho tayari m 5 inaweza ikausaidia kusimamisha boma tu na kupiga bati.
 
Mkuu garama za ujenzi pamoja na vifaa vya ujenzi dodoma vmepanda sana, kutokana na serikali kuhamia, M 5 Kwa Dodoma hiyo inatosha kununua kiwanja tu, labda kama kiwanja unacho tayari m 5 inaweza ikausaidia kusimamisha boma tu na kupiga bati.
Kiwanja kipo mkuu
 
Mkuu habari, samahani unaweza tuma mchanganuo wa kutokea chini kabla ya finishing
 
mkuu habari, samahani unaweza tuma mchanganuo wa kutokea chini kabla ya finishing
Sidhani kama nitakumbuka, sikuweka kumbukumbu kwa maandishi, nitajaribu.
Kujenga boma
1. Tofali 900@1,300
2.Mawe Lori za 4.5 m3 trip 3@130,000
3.Mchanga wa kokoto mweusi Lori 1=110,000 ( mbadala wa kokoto)
4. Mchanga laini Lori 5@150,000
5. Cement mifuko 45@ 14,500 mpaka plaster
6. Nondo 10mm.....sikumbuki I dad I
7. Mbao za lenta nilikodi @500/day
8.mbao za Bottom na malapa....~45,000
9.Mbao za kupaua na blandering/draft 130 PCs za 2.5M @ 6000
10. 34 pcs Bati za migongo mipana 30G @24,500
11. Fichaboard 94,000
12. Misumari
13. Madirisha 2 @ 115,000
14. Milango 4 @ 140,000
15. Fundi wa kujenga boma 600,000
16. Kupaua pamoja na draft 300,000
17. Fundi plaster na kufitisha milango na madirisha 320,000
 
Mkuu vp kuhusu vibali kutoka serikalini ni vp na vina gharimu kiasi gani?
 
🤔
 
Naomba ramani mkuu, Nina project ya ujenzi wa nyumba simple kama yako Dar
 
Mkuu vioo vya milango ni vipi?? Naona kama gharama nafuu Sana.
 
Nimekubal
 
Bei ya kiwanja kisasa n nzur sanaa kwann usifanye kujiongeza hiyo million tano tafuta kiwanja hata ihumwa au nala bei nafuu sana hata 1M unapata kizur afu cha kisasa unauza unajenga nyumba yako nzur kabisa n mtazamo tu
mkuu nasikia ihumwa pamekaa vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…