Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Mara nyingi wanajaaga wa upande wa mume ..wageni 5 mpaka 6 na wanakaa si chini ya miezi 6 ila upande wa mke akiomba hata ndugu yake kuja kusalimia baba mjengo anatia ngumu ila ndugu zake ruksa..baadhi ya wanaume wabinafsi sana
Nichangamoto kubwa sana
 
Dawa ya hapo mkuu ni kutafuta mashamba tu hata kama uko mjini! Kila asubuhi wakiamkia shamba lazima wasepe!
 
Daaah umenikumbusha kuna mchungaji mmoja hapa kitaa. Ndugu na watu wenye uhitaji wanaoishi pale kwake. Kawapatia mitaji ya kuuza mboga mboga,mua,kufuga kuku w nyama n mayai.wengine kutembeza juice na matunda. Hakuna anae poteza muda bure pale kwake. Ni mwendo w kuchapa kazi. Wapo wanao uza matango,nyanya,Nyanya chungu.
Vitu vya kuuza vinabadilika kutokana na msimu.
Nimemkubali mno pastor
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mbona China yenye 1.4B imetajirika na kuiacha Burundi yenye watu 10M, Malawi yenye 17M, Brazil yenye 200M, Russia yenye 140M?
 
Kinachomtajirisha ni uzalishaji na ubunifu. Hata mkiwa wawili tu lkn mnalala, hamzalishi, hakuna ubunifu, mtaendelea kuwa Maskini wa kutupwa.
 
Mkiwa hata 100 kwenye nyumba moja au compound moja lkn mnazalisha na kupangiana majukumu, hamtakamatika.
Mnachanganya mambo. Badala ya kuukabili uvivu, mnaukabili udugu na idadi. Udugu na idadi havileti umaskini. Sasa utasaidia kuondosha hasa ukitumiwa vizuri.
 
Nimesoma mawazo ya watu humu nimecheka sana ...ni kama mnazungumzia ofisini hamjafika site bado..hivi mnaosema kufukuza wageni mshakaa na wageni hata kwa miezi 6 wenye tabia tofauti ?Kama huna roho mbaya huwezi hata kithubutu kuwakoromea eti wakatafute..si ajabu wamekuja kujitafuta bado mambl hayajakaa sawa ya nn kuwafukuza..kama chakula kipo malazi yapo ya nn kuwafukuza mie akuuu kwangu wageni ruksa tena kama ni watafutaji wanaenda kupambana asibuhi naaandaa chai mwenyew kabla ya kuondoka wanapata kifungua kinywa murua kabisa waende shughuli zao wako full..sina baya Na mgeni mm
 
Wengine si watafutajii
 
Huwezi kufilisika kwa kusaidia badala yake utafunguliwa milango zaidi ya kupata pesa
 
Huwezi kufilisika kwa kusaidia badala yake utafunguliwa milango zaidi ya kupata pesa

Hiyo ni ahadi ya Mungu
 
Naunga hoja waache roho mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…