Kwa mlio karibu na Kibu Denis mpeni taarifa hii muhimu

Kwenye issue ya Feisal MBUMBUMBU yalipiga kelele kweli......lakini hii ya MVUTA BANGI....wananchi wala hatuna habari.
 
Nilivyoona Chama na Saido hawapo tena Simba nikajua wazi kwamba, Kibu hatofurahia maisha Simba. Na imekuwa hivyo.

Hawa watu walitengeneza ushirika hata wa kupasiana wenyewe mipira ya eneo la mwisho. Yaani walikuwa na timu yao ndani ya timu.

Hata ugomvi wa Chama na Ngoma, Kibu alijiingiza. Hii ni sawa na kisa cha kumlazimisha punda kwenda mtoni, na akagoma kunywa maji.

Wamwache aende.

Ova
 
Mchango wake ni mdogo! Wakati mnachezea kile kichapo cha goli tano ✊ ni yeye ndiye ambaye aliyewafungia angalau goli lile moja!?
Hamzitaki tena mbichi hizi eeh!? Kijani kaona mbali hataki tena kukumbwa na fedheha nyingine ya mwaka huu
 
Kiendacho kwa sangoma hakirudi. Tshs 400m hazirudiii. Ni mtaji wake huko ughaibuni
Unadhani ni rahisi hivyo kutokmea na hela za klabu?

Uwe unapata muda wa kujifikirisha usije kuonekana hamnazo kabisa mkuu.

Simba wanaweza kuanzia TFF kumshtaki Kibu kisha CAF then FIFA.

Anaweza kuamriwa arudishe fedha zote alizochukua za Simba na faini ya usumbufu pamoja na kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka.
 
Wewe akili huna kibu hachezi tena mpira utampatia wapi
 
Tatizo sio kutafuta pesa, kwanini aongeze mkataba ilhali anajua anatafuta timu?!

Mbona angetafuta timu akiwa mchezaji huru ingekuwa ina mashiko zaidi kuliko kusaini na kukacha kambi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…