Kwa mlio kwenye system, tujuzeni lile crane la tani 26 liliagizwa toka Sayari ipi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Eti jamani, kuna crane la tani 26 tuliambiwa ndio kikwazo cha kuanza kujaza maji kwenye Bwawa la Rufiji na limeagizwa toka nje ya nchi; Hivi mliposema nje ya nchi mlimaanisha nje ya sayari hii au ni vipi?

Miezi mingapi inahitajika kulileta hilo crane ambalo nchi nzima hii hakuna? Naomba majibu tafadhali
 
Linatoka Bukoba kwa wahaya yaani nshomile, litapita Uganda, Kenya halafu hukooo kwenu, tatizo mmeshaanza kuleta vi mdomo mdomo eti mna crane hadi za Tani 90, tunapanga majibu ya kuwapa na kundi la watu wa kushangilia majibu yetu, yule jamaa yenu si alishakufa, Sasa acha tule nchi huku mnatushangilia, mmeelewa
 
Mkuu usipojua kinaendelea nini huko Stiglaz, unaonekana irrelevant.
Crane haihitajiki kule, na kinachosubiriwa ni mageti ya kuzuia maji, na hilo halijazuia kazi ya ujenzi wa bwawa kuendelea.
Aaagh, sasa Makamba si kasema milango ipo tayari, ila winchi tu ndio shida, na linatoka nje ya nchi? Mbona mnatuchanganya lakini?!
 
Kwa bahati nzuri mimi nimefika Stiglaz na kuona maendeleo ya kazi.

Pressure ya kazi haipo kwenye kuzuia maji ili kutengeneza bwawa, pressure iko katika kuinua tuta la bwawa (Dam) na kujenga powerhouse itakayofungwa mitambo 9(turbines), kila turbine ikiwa na uwezo wa kufua umeme 235MW, au kwa turbine zote 9 , umeme utakaofuliwa ni 2115MW.

Haya masuala ya crane ni hype ya waandishi wa habari ambao hawana idea nini kinaendelea.
 
Sawa, ila hizo mashine hata zikifungwa zitaendeshwa na nini?! Si ni maji, sasa hayo maji si inabidi yajazwe, ndio tukaambiwa kujazwa ni hadi hilo crane lije ndio maji yajazwe, sasa Crane liko wapi?!
 
Muda wa kusimika hayo magate ya kuzuia maji haujafika.
Kama nilivyosema huko nyuma Power house ya mitambo haijakamilika sasa maji ya nini muda huu?
 
Maji yanaweza kujazwa hata kwa muda wa miaka miwili, sio kwamba yanajazwa leo kesho yamejaa; anyway, mimi ninachotaka kujua, hilo Crane liko wapi ili tuanze kujaza maji hilo bwawa? Wameliagiza sayari ipi? Jupiter au Mars?
 
Back
Top Bottom