Kwa mlio single huwa mna survive aje kipindi mnaumwa?

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Unaishi peke yako. Huna rafiki wa karibu, sasa ikatokea umepata Changamoto ya kiafya kama kuugua Ghafla usiku au kuumia bahati mbaya

Mnawezaje kupata usaidizi wa dharura?

Au ndio ile ku adapt na mazingira?

 
Kuumwa kihivyo sikuwahi, ila kuna siku nilipata hangover ya ulevi mpaka nilihisi nakata moto , kilicho niokoa nilijiburuza bafuni nikajifungulia maji yakanimwagikia , kidogo yalinipa nguvu ya kwenda kulipa tumbo chochote kitu ,nikapona.
 
Fikiria umeumwa serious kwa muda mrefu, unalazwa hospitali mara kadhaa, unarudi nyumbani kila baada ya wiki unatakiwa kwenda clinic. Una ndugu wakubwa kila mtu busy na familia yake, zaidi tu watakuja kukuona mara moja na kusepa kuwahi majukumu.
 
Naita bodaboda namba ninazo km zote plus manzi wa kufikia mara moja moja wa mtaani ambae nimezoeana nae kwa hio anaonekana km mke wangu mtarajiwa kumbe mara ya kwanza mara ya pili mara ya tatu
 
Dada wa kazi atakukokota kwenda bafuni kukusaidia kuoga? Atakuhudumia chakula wodini ukiwa umelazwa, atakukokota kwenda kwa daktari kupata vipimo, atafuatilia majibu ya vipimo ukiwa wodini?
Atakupeleka clinic?
Ndio maana tunasaka hela kwa bidii ila tuwe na madaktari na manesi binafsi bwasheee 😅


Uzuri mmjo ukiwa single kuumwa sio rahisi, kwa sababu hakuna wa kukupa stress za hapa na pale😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…