Ndio,ni ya mafanikio,ni wiki ya ushindi kwani kila mmoja wenu atapata mwenzie.Sasa zingatieni mambo yafuatayo:
A.Kwa wanawake wote mfanye yafuatayo:
1.Vaa vizuri kila utokapo nyumbani kwenda kazini,usivae nguo iliyofumuka au viatu vilivyosagika,kwa siku 7 mfulululizo vaa nguo za ndani mpya.Jipambe kwa marembo yote ya kike ambayo ni ya bei ya wastani,usivae vitu vya gharama kubwa
2.Zingatia sana usafi hasa usafi wa meno na mdomo,usafi wa nywele,makwapa yasitoe harufu kabisa
3.Uwe na uso wa furaha kwa kila mtu,na mchumba wako atakutafuta kwa kujifanya hana kitu,hivyo mpe tabasamu na maneno mazuri kila mtu,hasa unapokuwa approached na mwanaume aliyevaa vibaya vibaya,kwani huyo ndio mchumba wako,anakupima.
4.Usikae ndani,usijifungue kwani mumeo hayuko ndani kwako,yuko nje anakutafuta
5.Ukiendaa baa,usiwe mropokaji,usiongee sana,usilewe sana,usiwe unakula kama uko kwenye vita.
6.Kama baba yako mzazi yupo hai,ongea nae,mwambie baba natafuta mchumba,nisaidie,baba yako mzazi anao ufunguo wa wewe kupata mume
7.Panga vigezo vya mchumba umtakae vizuri,usiweke vigezo vigumu hutafanikiwa
B.Kwa wanaume,zingatia yafuatayo:
1.Unatafuta mwenza wa maisha,hutafuti malaika
2.Jichanganye na watu sana,ili ukutane na wanawake wengi upate kuchagua
3.Tengeneza vigezo vya mchumba umtakae kwanza na mshirikishe mama yako sana.
4.Kwa sasa kuna wimbi la wanawake kutoka nje ya nchi wanataka kuolewa na watanzania,changamkia hilo suala
5.Kumbuka unatafuta mke sio malaika
6.Tembea,toka ndani,jichanganye na watu,uwe mchangamfu,ukimuona mwanamke na roho ikakupige pwaaaaaa,mfuatilie na uwe mvumilivu
7.Ndani ya siku 7 ukikutana na mdada ana umbo zuri ila kavaa mradi mradi,mfuatilie kwani huyo ndio mkeo
ASANTENI