Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Usiniambie mkuu yani pale Berlin wali ndondo ni Buku?
Haipo hivyo ila bia supermarket ni kama Bongo au cheep zaidi.. Halafu kwa uchumi wa Ujerumani hiyo pesa ya bia ni kama sh. 100 tuu haiumizi yani bia ipo bei chini kuliko kilo ya mchele au robo kilo ya karanga.. So unaweza kuelewa

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Usihamishe magolinya kariakoo ukayapeleka ulaya kwanza angalia Uchimi wao.ndio tuanzie hapo pia tuimia elimin'dogonya exchange rate usitishe watu
One Norwegian Krone equals
277.99 Tanzanian Shilling
 
Wapo Africans wengi, unakula mkenya, akizubaa unakula mnaija hivyohivyo wazungu ni ngumu labda wale wa kujiuza
Mkuu unaogopa unyanyapaa kutokea demu wa kizungu, au utakuwa unaogopa kupewa msala wa sexual harassment urudishwe bongo mkuku mkuku.....
 
Moja ya swali ambalo nimeulizwa Sana na wadau humu Ni kuhusu chakula.

Imenibidi nijibu hili kwa kuweka post maana Kuna Mtu amesema yeye amefanya kila aliwezalo kuja na amefanikiwa kwa 90%(anajua mwenyewe kafanyaje) maana yeye ni Mtu anayependa kula na kupiga gambe.

Mimi mwanzo kabisa nilipoingia niseme wazi nilipata changamoto kubwa Sana ya chakula, ulikuwa mtihani Ila baada ya muda nilizoea vyakula vyao na gharama zake taratibu.

Hivyo ni vyema nikaeleza Hali halisi ili Mtu ajue kupoje kwenye suala la chakula huku.
Huku hakuna mama ntilie au mgahawa bubu ambapo utaingia na sh.2000 utaondoka umeshiba, la hasha huku kwenye msosi kuna migahawa ambayo ni ya hadhi kidogo na bei imechangamka ukitaka kula na kushiba andaa 60000 hadi 80000, elfu sitini Hadi elfu themanini.

Karibu vyakula vingi vinapatikana ni pesa yako tu.

Nakutolea mfano tu: kilo ya mchele huku ni Kati ya Tshs 6000 - 8000, na kilo ya nyama ni Kati ya Tshs 70000 - 90000. Yes ni elfu sabini hadi elfu tisini(natamani bongo iwe hivi ili watu waheshimiane)

Hivyo kula wali nyama ni anasa, Mimi chakula changu kikubwa ni mikate, sausage, maziwa, samaki, chips n.k.

Maji ya kunywa Mara nyingi nikienda kwenye kazi nachota ya bomba, ni masafi na mazuri Sana Ila ukitaka kununua ya chupa ni sawa pia.

Kuhusu beer Kuna gharama kidogo Ila bei ni sh.8500 kwa baadhi ya bia na nyingine ni zaidi ya hapo, hadi heineken zipo Ila ni sh 12000. Na pia soda pepsi zipo bei ni humohumo 8500

Suala la mwisho ambalo ungependa kujua ni gharama za ninapoishi, ni chumba kimoja Cha kulala na gharama ni million 2 kwa mwezi.

Nahisi nitakuwa nimejibu maswali ya wadau wengi pamoja na aliyeniuliza.
Chini ni picha moja ya mgahawa nikiwa na maji ya Farris, na vyakula ndani ya huo mgahawa.

Picha nyingine ni bar, huku hata ukiwa bar hakuna kujuana kila mtu afanye mishe zake, hawapendi kabisa kupiga story na mtu wasiyemjua.
Sasa ndugu yangu kama ni hvyo kumbe hata mimi naweza kukomaa huko mchele 1kg 7000, hapo utakua ni mwendo wa wali mkavu na chai au maji ya bomba kama ulivyoainisha mkuu😄😄😄😄😄
 
Wapo Africans wengi, unakula mkenya, akizubaa unakula mnaija hivyohivyo wazungu ni ngumu labda wale wa kujiuza
Ina maana mkuu mpaka sahiv hujala papuchi ya kizungu, we n wakenya tu na nigerians?
 
Mkuu umeweka figure kwa Tshs maisha yanaonekana ghali kwa sababu ya thamani ya Tshs iko chini sana. Mfano miaka ile ya 1980 ungemwambia mtu kuna siku tutanunua sukari kilo Tshs 6,000/= . Nawashauri wale wenye ndoto za kwenda huko msikate tamaa
 
Back
Top Bottom