Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji



Alafu ajabu watu kama wewe mnarudi!...harufu ya umaskini inakera mno aise
 
Hizo hela ukibadili ki tsh ni shilingi ngapi?? Mfano 70000 huku ni sh ngapi?? Au 8500 kwa hela yabongo ni sh ngapi?
 
Asubuh chapati mbili jero na supu ya mapupu ya mia tatu, mchana ugali dagaa, maharage, mchicha na kachumbar kwa buku, ahaaa bongo tam babu
 
Alafu ajabu watu kama wewe mnarudi!...harufu ya umaskini inakera mno aise
Weweee! heri kuishi kwako penye sakafu ya vumbi kuliko kuishi kwenye nyumba yenye tiles ya kupanga yenye masimango. Ila majamaa unaweza kufikiri hapo ulaya ndo peponi, hewa utafikiri magari hayatoi moshi kama upo kijijini vile, vumbi utalitafuta kwa tochi nilienda na brush yangu na kiwi sikuwahi hata kuvitumia na sikuwahi kujua mifereji ya maji wala line za umeme zinapita wapi...
 
Kama per capita income yao ni kubwa naona ni sawa, otherwise wangekua washaikimbia nchi yao
 
Dah,hii imenitafakarisha,nikifikiria nimeingia kwa mama ntilie asubuhi hii,nimepiga chai ya rangi 300,viandazi vitano each 200,total nimetumia 1300 kwa breakfast,na ninahisi kijasho kinanitoka,kwakweli huko kaeni tu wenyewe...
 
We bwana.....ngoja tukaolewe tu huko sasa ..!
 
Nimecheki kwenye hii link kweli bei unazotaja na zimechangamka ndio maana mtu anakaa majuu anapata labd usd 5000 kwa mwezi ila hawezi hata kufanya savings gharama za maisha zipo juu sana, anaishi maisha mazuri lakini "hand to mouth". Akija bongo anarudi na minguo tu na vitu vya ndani pengine na maarifa kwa wajanja.

Kama unafursa ya maana ndani ya africa ni bora zaidi kuliko huko ulaya, mfumo umetengenezwa kukufanya uzalishe na utumie kukuza uchumi wao.

 
Gharama za maisha kwa mtu wa kawaida ulaya haziko juu saaana, kwa infrastructures walizokwishaweka na teknolojia za kisasa walizonazo kwenye mambo ya uzalishaji wa vyakula na kutoa huduma mbalimbali unafanya gharama ziwe chini, sema itategemea unaishi kwenye jiji gani na eneo unalokaa. Mfano, kama unaishi kwenye mji mdogo au umepanga nje ya jiji (sub-urban areas) unaweza usione hizo gharama na utafanya savings za kutosha kuweza kujenga mjengo hata kununua gari la kisasa kabisa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…