Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Bongo iwe hivi watu waheshimiane
Sasa embu toa ufafanuzi kidogo uthamani wa hiyo hela ya huko dhidi ya kwetu, maana unazidi tu kunichanganya.

Wanatumia uero ama kitu gani na hudai kuwa inathamani sana kuliko yetu!

Sasa kwa mwendo huo wa kununua kilo ya nyama tisini elfu, hiyo hela inaizidije thamani shilingi ya Tz, kama kwenda kwenye manunuzi mpaka uwe na sandarusi la pesa, wakati Tz noti1 elfu10 unarudi na chenji?
 
Moja ya swali ambalo nimeulizwa Sana na wadau humu Ni kuhusu chakula.
Imenibidi nijibu hili kwa kuweka post maana Kuna Mtu amesema yeye amefanya kila aliwezalo kuja na amefanikiwa kwa 90%(anajua mwenyewe kafanyaje) maana yeye ni Mtu anayependa kula na kupiga gambe.

Mimi mwanzo kabisa nilipoingia niseme wazi nilipata changamoto kubwa Sana ya chakula, ulikuwa mtihani Ila baada ya muda nilizoea vyakula vyao na gharama zake taratibu.

Hivyo ni vyema nikaeleza Hali halisi ili Mtu ajue kupoje kwenye suala la chakula huku.
Huku hakuna mama ntilie au mgahawa bubu ambapo utaingia na sh.2000 utaondoka umeshiba, la hasha huku kwenye msosi kuna migahawa ambayo ni ya hadhi kidogo na bei imechangamka ukitaka kula na kushiba andaa 60000 hadi 80000, elfu sitini Hadi elfu themanini.

Karibu vyakula vingi vinapatikana ni pesa yako tu.

Nakutolea mfano tu: kilo ya mchele huku ni Kati ya Tshs 6000 - 8000, na kilo ya nyama ni Kati ya Tshs 70000 - 90000. Yes ni elfu sabini hadi elfu tisini(natamani bongo iwe hivi ili watu waheshimiane)

Hivyo kula wali nyama ni anasa, Mimi chakula changu kikubwa ni mikate, sausage, maziwa, samaki, chips n.k.

Maji ya kunywa Mara nyingi nikienda kwenye kazi nachota ya bomba, ni masafi na mazuri Sana Ila ukitaka kununua ya chupa ni sawa pia.

Kuhusu beer Kuna gharama kidogo Ila bei ni sh.8500 kwa baadhi ya bia na nyingine ni zaidi ya hapo, hadi heineken zipo Ila ni sh 12000. Na pia soda pepsi zipo bei ni humohumo 8500

Suala la mwisho ambalo ungependa kujua ni gharama za ninapoishi, ni chumba kimoja Cha kulala na gharama ni million 2 kwa mwezi.

Nahisi nitakuwa nimejibu maswali ya wadau wengi pamoja na aliyeniuliza.
Chini ni picha moja ya mgahawa nikiwa na maji ya Farris, na vyakula ndani ya huo mgahawa.

Picha nyingine ni bar, huku hata ukiwa bar hakuna kujuana kila mtu afanye mishe zake, hawapendi kabisa kupiga story na mtu wasiyemjua.

View attachment 1806118View attachment 1806119View attachment 1806120View attachment 1806122
Hii thread iko kitapeli mnoo.
Kuna watu wanakwenda kutapeliwa hapa JF kiulaini sana.

Kwa kuwasaidia baadhi ya watu hapa JF ambao hawajawahi kufika ulaya, taarifa nzima ya gharama na mfumo wa maisha ya eneo lolote husika katika nchi ya Norway inaweza kuipata kwa usahihi wa karibu 99% kwenye mitandao ya taarifa rasmi za nchi ya Norway. Unaweza kujua hata bei ya kununua changadoa na ukapewa, huhitaji kuja kulishwa matango pori ya wajanja na matapeli wa hapa JF.

Kwa mfano kupitia websites za;
-numbeo.com
-fullsuitcase.com
 
Hahaha fafanua kidogo hapo nilipoweka wino mzito.
mzee umasikini unanukia, sio kwenye nchi tu , hata familia au nyumba fulani ukienda na kukaribishwa ndani, hali ya hewa tu mle ndani inaweza kukupa jibu kuwa nyumba hii umasikini umetapakaa (roho ya umasikini), umasikini ni roho na inaweza kutambuliwa kwa lugha ya kiroho (discerning in the spirit). utajiri vilevile, kuna hali inakuambia na kwa uhakika kuwa mji huu ni wa kitajiri, nyumba hii ni yakitajiri, mtu huyu ni tajiri au masikini etc., mtu huyu ni mwema, mtu huyu ni hatari, mazingira haya ni hatari au salama au yana huzuni etc.
 
Mi nataka kazi, wangari ndio anatafuta ndoa....
Hahahahhahaa umenilabel aise...hhaha...education is sexy😀😀!
Kuna dini fulani wanasemaga ukiolewa UNASITIRIKA! huwa sielewi maana ya kusitirika !
_jisitiri(li)? Naonaga linatumika kama ujisitiri kimavazi vile ??ah sijui bwana .acha nikasitirike majuu!😒
 
Back
Top Bottom