Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Kwa mnaotaka kuja Norway, ujipange kwa vyakula na vinywaji

Siye akina baba ni aibu kutoka kwako kwenda kushobokea kwa jirani, nyie akina mama ruksa ila msije kurudi mnalialia mkikuta nafasi zenu zimejazwa na mibebezi ya kutoka Eritrea...
 
Siye akina baba ni aibu kutoka kwako kwenda kushobokea kwa jirani, nyie akina mama ruksa ila msije kurudi mnalialia mkikuta nafasi zenu zimejazwa na mibebezi ya kutoka Eritrea...
Naona tunaanza kutishwa sasa jamani! Saitakuaje
 
Nipe tenda nikupige ngeli, usipo tema yai kama Theresa May nakurudishia pesa yako.
🤣🤣! Napiga shortcut ya kunywa tu daily ung'eng'e ushuke hiyo fee ya ngeli bora nikanunue kijora cha kumtega mume😀
 
Moja ya swali ambalo nimeulizwa Sana na wadau humu Ni kuhusu chakula.
Imenibidi nijibu hili kwa kuweka post maana Kuna Mtu amesema yeye amefanya kila aliwezalo kuja na amefanikiwa kwa 90%(anajua mwenyewe kafanyaje) maana yeye ni Mtu anayependa kula na kupiga gambe.

Mimi mwanzo kabisa nilipoingia niseme wazi nilipata changamoto kubwa Sana ya chakula, ulikuwa mtihani Ila baada ya muda nilizoea vyakula vyao na gharama zake taratibu.

Hivyo ni vyema nikaeleza Hali halisi ili Mtu ajue kupoje kwenye suala la chakula huku.
Huku hakuna mama ntilie au mgahawa bubu ambapo utaingia na sh.2000 utaondoka umeshiba, la hasha huku kwenye msosi kuna migahawa ambayo ni ya hadhi kidogo na bei imechangamka ukitaka kula na kushiba andaa 60000 hadi 80000, elfu sitini Hadi elfu themanini.

Karibu vyakula vingi vinapatikana ni pesa yako tu.

Nakutolea mfano tu: kilo ya mchele huku ni Kati ya Tshs 6000 - 8000, na kilo ya nyama ni Kati ya Tshs 70000 - 90000. Yes ni elfu sabini hadi elfu tisini(natamani bongo iwe hivi ili watu waheshimiane)

Hivyo kula wali nyama ni anasa, Mimi chakula changu kikubwa ni mikate, sausage, maziwa, samaki, chips n.k.

Maji ya kunywa Mara nyingi nikienda kwenye kazi nachota ya bomba, ni masafi na mazuri Sana Ila ukitaka kununua ya chupa ni sawa pia.

Kuhusu beer Kuna gharama kidogo Ila bei ni sh.8500 kwa baadhi ya bia na nyingine ni zaidi ya hapo, hadi heineken zipo Ila ni sh 12000. Na pia soda pepsi zipo bei ni humohumo 8500

Suala la mwisho ambalo ungependa kujua ni gharama za ninapoishi, ni chumba kimoja Cha kulala na gharama ni million 2 kwa mwezi.

Nahisi nitakuwa nimejibu maswali ya wadau wengi pamoja na aliyeniuliza.
Chini ni picha moja ya mgahawa nikiwa na maji ya Farris, na vyakula ndani ya huo mgahawa.

Picha nyingine ni bar, huku hata ukiwa bar hakuna kujuana kila mtu afanye mishe zake, hawapendi kabisa kupiga story na mtu wasiyemjua.

View attachment 1806118View attachment 1806119View attachment 1806120View attachment 1806122
Aisee Acha niendelee kula Chips kwa Eddo 🚶🏽‍♀️
 
Kilo ya nyama elfu 70-90...sema umeandika kwa vitisho sana....kama muvi za kutisha.
 
Hakuna kitu bei chee Ulaya kama chakula! Nchi nyingi za Ulaya hasa EU zina standard moja ya maisha,tofauti ni ndogo sana. Sijafika Norway ila sidhani kama kilo ya nyama inafika 70,000! Nakumbuka enzi tunapiga box nyama ya kuku tulikuwa tunanunua kwenye box unachagua mapaja au vidari na box kubwa sana tunakula wiki nzima watu watano na wageni wakitokea, box lilikuwa £12, mchele Basmati kg5 ilikuwa £12-15,nyama lamb kilo £3 hivi nyama ya ng'ombe iko juu kama £4 kwa kilo au zaidi kidogo, mazagazaga mengine mostly kwenye makopo kwenye supermarket majuisi,yoghurt,etc bei chee tu. Kwa mishahara ya kubeba box hata minimum wage huumizi kichwa kwenye kula,kuvaa,kulala ndio maana unaona watu wakitoka majuu kuja bongo wanang'aa sana hata kama hawana hela za kujenga magorofa.
 
Back
Top Bottom