Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, ameendelea kukonga mioyo ya mamilioni ya watanzania kwa moyo wake wa upendo,huruma ,kugusa Maisha ya watu,kuwajali wanyonge na kujinyenyekeza kwa watu.
Ameendelea kuonyesha namna Maisha yake hapa Duniani yalivyo kwa ajili ya kuleta tabasamu, furaha ,matumaini,nuru na kuwaangazia na kuwamulikia watu Mwanga.ameendelea kuwa muwezeshaji na mfanikishaji wa ndoto za watu.ameendelea kukata kiu na kuwafuta machozi watu.
Katika muendelezo wa kazi hiyo iliyotukuka na njema na iliyobarikiwa mbele za Mwenyezi Mungu.Ameweza kumimina kiasi cha shilingi Millioni 425 katika wilaya ya Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kijamii.Ambapo kiasi cha Millioni 300 kati ya Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa kituo cha afya Matiani.
Hii ikiwa na maana kuwa RAIS wetu mpendwa ambaye Ni Mama mwenye watoto,wajukuu anatambua umuhimu wa huduma za afya kuwepo karibu.ili wapate huduma pasipo kusafiri umbali mrefu kwa mama wajawazito,watoto,wazee na watu wenye maradhi mbalimbali.
Hataki watu wapoteze maisha kwa kukosa kituo cha afya au huduma za afya au kuona akina mama wakijifungulia majumbani na kuhatarisha Maisha yao au kuona watu wanapoteza maisha na kufia njiani kwenda wilaya zingine kutafuta huduma. Mama yetu na Rais wetu ndio maana ameamua kufanya haya kwa kutoa pesa hizo.
Ambapo zingine pia zitakwenda katika ujenzi wa daraja na zingine katika ukarabati wa barabara inayounganisha kata ya Matiani na ofisi za halmashauri.hii ikiwa na maana kuwa anataka kuwarahisishia wananchi hao kufika kwa urahisi na uharaka kupata huduma katika ofisi za halmashauri bila shida.
Kwa hakika Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi ni Mtumishi wa kweli wa watanzania,Ni Muwezeshaji wa watanzania,ni mfanikishaji wa ndoto za watanzania.Anafanya na kupeleka huduma kwa wananchi pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile. kwa hakika ikiwa tutashindwa kutambua mchango wa Rais Samia Hapa Nchini,basi Mungu atamlipa Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya kwetu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.