bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Msipofanna nyota bila Mungu sahauni kudumu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani ndoa inakuwa na sarakasi za kutosha ikionekana huelewi Ndugu mwanaume unapelekwa mahakamani kwa kesi ya ulawiti au ubakaji kule nako unakuta yupo Mwanaharakati anakugonga nyundo. Tayari ndoa imeisha hiyo.Wanatamani ndoa wakishazipata wanaanza Tena kupambana kuzibomoa,
umenikumbusha familia moja waliishi pamoja ile 'sogea tukae' miaka zaidi ya 8, wakaja kufunga ndoa haikudumu hata miezi ikavunjika..!!Kuna watu walikaa kwenye mahusiano miaka 8 wakaja funga ndoa mwezi tu chali sijuagi huwa wanakumbwa na vitu gani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi ndoa Mungu atusaidie kwa kweli. Huyu dada wa huku baada ya ndoa kuvunjika kakaa kidogo akazaa na jamaa mwingine yupo tu anajilelea katoto kake.umenikumbusha familia moja waliishi pamoja ile 'soge tukae' miaka zaidi ya 8, wakaja kufunga ndoa haikudumu hata miezi ikavunjika..!!
Watu na kampeni zao za kataa ndoa
Ukweli mchungu, mi nafikiri muishi kwanza, mpate hata mtoto mmoja, ndio tufanye sherehe,Bora ndoa za, mkataba, au utoaji taraka urahisishwe, fikiria, mke anakuta SMS ya mapenzi, kwenye cm, anakuvizia umelala, anakuminya nyeti! And kudunga kisu cha kifua! Unakurupuka, unatembeza kipigo mpaka unazidiwa, wote mnakimbizwa hospitari mahututi, mume anakufa, mama yupo hoi, na pingu mkononi! Watoto mmemuachia nani,? Hapo watoto shule ndio basi, mateso,kunyanyasika, kama mtoto wa kike, ataishia kuwa danga,wa kiume kibaka, au shoga!Yaani ndoa inadumu muda mfupi kuliko hata ule uliotumika kwenye vikao??
Kuna haja ya watanzania kubadilika ktk suala hili la sherehe za harusi. Tafakari ya kina ifanyike ili tuchukue mwelekeo mpya.
Watu wafunge ndoa kwenye nyumba za Ibada na baada ya hapo waelekee majumbani mwao na siyo kwenda kwenye kumbi kufanya maigizo ya kujifaharisha.
Mnafanya maonesho ukumbini ya fahari kubwa na kujifanya mna furaha kubwa kumbe watu wenyewe hata hampendani.
Kuna ndoa nimechangia laki 2 zangu lkn imedumu siku 21 tu.
Sisi sisi au wengine babu?Wana Jf....
Nawaomba muendelee kuiombea ndoa yetu idumu kwa furaha na amani tele tulio nayo hii...😊
maskiini..!!Hizi ndoa Mungu atusaidie kwa kweli. Huyu dada wa huku baada ya ndoa kuvunjika kakaa kidogo akazaa na jamaa mwingine yupo tu anajilelea katoto kake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Daah! Kiukweli watoto wanaingia kwenye kisima cha mateso pasipo kutarajia.fikiria, mke anakuta SMS ya mapenzi, kwenye cm, anakuvizia umelala, anakuminya nyeti! And kudunga kisu cha kifua! Unakurupuka, unatembeza kipigo mpaka unazidiwa, wote mnakimbizwa hospitari mahututi, mume anakufa, mama yupo hoi, na pingu mkononi! Watoto mmemuachia nani,? Hapo watoto shule ndio basi, mateso,kunyanyasika, kama mtoto wa kike, ataishia kuwa danga,wa kiume kibaka, au shoga!
Wiki 3!!! Inatokeaga hasa chanzo kikuu ni usaliti
Kuna mzee mmoja jirani yangu huwa anatoa nadharia hii. Anasema harusi ndiyo inakaribisha ulozi, mikosi na mabalaa mbalimbali. Anatolea mfano kwa kusema kuwa utakuta watu wameishi kinyumba kwa miaka hata 5, lkn wakifunga ndoa na kufanya harusi tu migogoro inaanza.Kupiga parange kutaka hela za watu wakuchangie harusi unakaribisha manuksi, mikosi na mabalaa. Wengine hela zao za mashetani alafu unachukua kuchangia tendo takatifu la ndoa?? Unamkaribisha shetani kwenye ndoa yako! Usihusishe watu wasio wa muhimu katika ndoa yako hasahasa kutaka hela zao! Lipa mahari, pata ridhaa ya wazazi, nenda kanisani au serikalini (tendo la kisheria la umiliki wa mwenza) chukua mkeo nenda nyumbani! Hao unaowahusisha na kula hela zao wengi wachawi!
Unakutana na hakimu mwanamke aliyevurugwa na ndoa lazima uchezee miakaYaani ndoa inakuwa na sarakasi za kutosha ikionekana huelewi Ndugu mwanaume unapelekwa mahakamani kwa kesi ya ulawiti au ubakaji kule nako unakuta yupo Mwanaharakati anakugonga nyundo. Tayari ndoa imeisha hiyo.
Wanaopenda hawahitaji gharama kubwa kuonesha furaha yao.Mnafanya maonesho ukumbini ya fahari kubwa na kujifanya mna furaha kubwa kumbe watu wenyewe hata hampendani.
Hahaha ndio yule alimkamua Mama wa watu maskini Kule Iringa Miaka 20 eti kala nyama ya mnyama pori haifiki hata kilo mbili.Unakutana na hakimu mwanamke aliyevurugwa na ndoa lazima uchezee miaka