Kwa mparaganyiko huu wa ndoa, sitaki tena kusikia wala kupokea kadi ya mchango wa harusi tena

Kwa mparaganyiko huu wa ndoa, sitaki tena kusikia wala kupokea kadi ya mchango wa harusi tena

Ndio maana mimi ikiwezekana nitampanga bibie tukamalizie mambo bomani, asubuhi tunaenda zetu bomani tukitoka tunapita KFC kupata kuku na coke kubwa then tunaenda beach kuogelea, tunarudi home kulala.
Kesho yake Tunaingia zenji siku 3. Sherehe na honeymoon inakua imeisha hivyo.
Kwani bomani si ni ndoa? Ndoa maana yake ni muunganiko wa "kisheria" unaotambulisha kuwa hawa ni mme na mke na wanakuwa na cheti. Cheti kinatolewa na serikali hata kama ndoa ya kanisani/msikitini/bomani. Kanisani tunatafuta "baraka" za huyo unayemwabudu aingilie kati na kuwalinda/kuwabariki. Usipofanya hivyo shetani anachukua usukani!
 
Yaani ndoa inadumu muda mfupi kuliko hata ule uliotumika kwenye vikao??

Kuna haja ya watanzania kubadilika ktk suala hili la sherehe za harusi. Tafakari ya kina ifanyike ili tuchukue mwelekeo mpya.

Watu wafunge ndoa kwenye nyumba za Ibada na baada ya hapo waelekee majumbani mwao na siyo kwenda kwenye kumbi kufanya maigizo ya kujifaharisha.

Mnafanya maonesho ukumbini ya fahari kubwa na kujifanya mna furaha kubwa kumbe watu wenyewe hata hampendani.

Kuna ndoa nimechangia laki 2 zangu lkn imedumu siku 21 tu.
Mimi ya mshikaji wangu imedumu miezi 3 jana kila MTU kaelekea njia yake!
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Kupiga parange kutaka hela za watu wakuchangie harusi unakaribisha manuksi, mikosi na mabalaa. Wengine hela zao za mashetani alafu unachukua kuchangia tendo takatifu la ndoa?? Unamkaribisha shetani kwenye ndoa yako! Usihusishe watu wasio wa muhimu katika ndoa yako hasahasa kutaka hela zao! Lipa mahari, pata ridhaa ya wazazi, nenda kanisani au serikalini (tendo la kisheria la umiliki wa mwenza) chukua mkeo nenda nyumbani! Hao unaowahusisha na kula hela zao wengi wachawi!
Pokea 🌺💐🪷🪻🌷⚘️🌹🌻yako hela zao za maagano, na macho yao ya husda hiyo ndoa haitoboi
 
Rafk angu wa karibu sana ....amefunga ndoa kesho asubuh ilibd tuende hospital kumchek mgonjwa fulan wa muhim sana....tulipotoka hospital jamaa akaenda kula mzgo mchepuko...jamaa alifunga ndoa ya gharama ya KIJESHI ... Kwakwel KATAA NDOA..
Nb: alisahau kadi ya benk so hela ya lodge nlitoa mm ..
 
Ex ni janga la kimataifa mkuu

Ex hawaepukiki. Maana siku hizi tunachelewa kufunga ndoa kwa sababu kibao.

Huwezi kuoa binti wa miaka 28 ambaye hana X zake.

Na huwezi kuolewa na mwanaume wa miaka 28 ambae hana X zake.

Imagine hao wa miaka 28 ndio wanaonekana wamewai kuolewa ama kuoa.

Ndoa nyingi siku hizi maharusi wanakuwa above 30.

Je kuna mtu wa hizo age ambaye hana ma X wake ?

Ukitaka kuoa mwanamke ambaye hana X zake. Muwai umuoe akiwa na miaka 18, ama 20
 
Ex hawaepukiki. Maana siku hizi tunachelewa kufunga ndoa kwa sababu kibao.

Huwezi kuoa binti wa miaka 28 ambaye hana X zake.

Na huwezi kuolewa na mwanaume wa miaka 28 ambae hana X zake.

Imagine hao wa miaka 28 ndio wanaonekana wamewai kuolewa ama kuoa.

Ndoa nyingi siku hizi maharusi wanakuwa above 30.

Je kuna mtu wa hizo age ambaye hana ma X wake ?
Sijabisha isome tena hiyo comment
 
Kwani bomani si ni ndoa? Ndoa maana yake ni muunganiko wa "kisheria" unaotambulisha kuwa hawa ni mme na mke na wanakuwa na cheti. Cheti kinatolewa na serikali hata kama ndoa ya kanisani/msikitini/bomani. Kanisani tunatafuta "baraka" za huyo unayemwabudu aingilie kati na kuwalinda/kuwabariki. Usipofanya hivyo shetani anachukua usukani!
Maana yangu ni kwamba nataka kitu simple.
 
Kuna mzee mmoja jirani yangu huwa anatoa nadharia hii. Anasema harusi ndiyo inakaribisha ulozi, mikosi na mabalaa mbalimbali. Anatolea mfano kwa kusema kuwa utakuta watu wameishi kinyumba kwa miaka hata 5, lkn wakifunga ndoa na kufanya harusi tu migogoro inaanza.
This makes sense unajua. Kiukweli ndicho kinachotokea.
 
This makes sense unajua. Kiukweli ndicho kinachotokea.
Kabisa mkuu. Haiwezekani watu waishi kwa amani wakati wa sogea tukae miaka hata 8. Wakifanya tu harusi migogoro inaingia.
 
Back
Top Bottom