Kwa mpira wa jana mapengo ya Chama na Miqueson yapo wazi

Nahisi wewe tayari ushapokea bahasha ya kaki
 
Mpira umevamiwa jamani. Mleta mada kavamia tu mpira lakini kiukweli mpira haujui kabisa. Watu wanaojua mpira wanaelewa kuwa watu kama Chama na Luis hutokea mara chache sana na ndio maana ikawa vigumu sana kwa Simba kuwazuia wasiondoke kwa sababu timu kubwa nyingi zilikuwa zinawahitaji kwa udi na uvumba. Chama ni chama tu na Luis ni Luis tu huwezi kuwafananisha na wachezaji wengine kwani kila mtu ana kipaji chake binafsi. Hao wakina Banda na Sakho nao wana vipaji vyao tofauti na staili zao za kuchezaji. Kwa hiyo mleta mada kutaka wachezaji wapya wa Simba ndio wawe kama walivyokuwa wanacheza Chama na Luis kwa asilimia 100% huo ni ujuha. Swala la kuwa wameacha pengo au hawajaacha pengo hilo ni suala mtambuka sana na ni mapema sana tusubiri walau Simba wacheze angalau mechi 10 za mashindano ndio watu watoe tathmini zao.
 
Timu haikua na utulivu, inshort walikua wanafika ruka tu, kwa sasa simba tunahitaji utulivu sana ili team yetu ipate muunganiko
hili ni linyani na utopolo lisiwaumize vichwa kujaza komenti kwenye post yake yakitopolo
 

Mkuu Simba Walijidanganya ETI wanafanya Biashara eti kuna watu wanaojiita Maarufu wakashauri wauzwe....
Sasa Unauza unaziba na Nani?
Una Mbadala?
Ndio Maana Kuna Kupindi Messi akikuwa hauzwi kwa gharama yeyote pale Barcelona Kwa miaka yote,Mpaka Juzi baada ya Barca kuwa wamejiridhisha wamechukua makombe ya Kutosha Malengo yanefikiwa na Mbadala yupo,
Wao eti Aanajidanganya Mpira Biashara[emoji3063][emoji3063][emoji51][emoji51]
Kuna Tumubzinakuambia Kabisa Msimu huu hauzwi Mtu labda Msimu Ujao kama Hawajajiandaa!
Ukiuliza sana Wanakuambia Alikuwepo Samatta Kauzwa,Arsenal alikuwepo Henry Kauzwa.Strategies zinabadilika ndio Maana Kuna Kipindi Bayern huwagusi kwa Robert Lewandoski mwaka huu ndio jamaa ameomba kuondoka After 4-5years pale.
Sasa Wameuza mapengo tena Makubwa yameonekana wanabaki kujiumauma tuu!
Atleasr wangewauza Mwakani halafu Mwaka huu ikawa ni Kutafuta Mbadala tuu!
Ina sasa wameleta ugoro tuu!
Wanakuwa kama mwanamke mwenye shida ya Hela hawezi kataa Mwanaume mwenye hela
 
Acha unafki wewe,, umekaza mku#@€€ndu kuandika gazeti,, hiyo mechi we umeangalia wapi?,, Na pia hata huyo miqquison wakati anakuja hakushain mechi ya kwanza tena alikuwa anaanzia bench halikadhalika chama,, sasa wewe/nyie utaputapu fc huruma na simba mmeanza lini mpaka mlalamike kuhusu chama&miq wakati simba wenyewe wapo kimya na mjadala huo washaufunga kama si unafki.
 
Mbadala wa Messi pale Barca wamempata nani ?

Hivi Messi kauzwa au kamaliza mkataba wake ?
 
Wamewashushua balaa , na ni kweli Simba wapo vizuri zaidi mitandaoni na taarifa nyingi wanazipatia mitandaoni so hayo magazeti ya waandishi wasiozingatia ueledi lazima yalalamike tu
 
Eti nini Barca wamepata mbadala wa Messi. Kuna Messi mmoja tu hapa duniani kama ilivyo kwa Christiano Ronaldo, kama ilivyo kwa Ronaldino Gaucho full stop". Sana sana watakuja wengine kwa staili zao za uchezaji na watakubalika. Kwa hiyo hata Simba usitegemee eti kuna mchezaji atakuja kuwa kama Chama au Miquisone. Hapo Simba walipita miamba kama Hamis Gaga, Malota Soma, Hussein Masha, Mafisango na wengineo lakini ni nyakati tu zinatufanya tuone kuwa bila Chama na Luis Simba haiwezi kwenda.

Naamini kabisa watakuja wachezaji wengine watafanya vizuri na ikifika wakati wanaondoka habari zitakuwa ni hizi hizi tutasema tena kwa nini fulani na fulani wanaondoka. Tusiwape presha wachezaji wapya ili wafanane na Chama au Luis badala yake tuwape muda ili nao waache alama zao kwa kupitia vipaji vyao na aina zao za uchezaji. Suala la kuondoka Chama na Luis sidhani kama uongozi uliridhia kwa urahisi kwani hata wao wangependa wabaki Simba muda mrefu lakini nafikiri wachezaji wenyewe walishaamua kuondoka. Na duniani kote mchezaji akiamua kuondoka huwezi kumzuia vinginevyo uamue tu kuua kipaji chake umweke benchi msimu mzima maana ukimchezesha tu atakuwa anakuchomesha halafu hasara kwa nani?. Na mkataba ukiisha anaondoka bure kabisa sasa hiyo itakuwa ni akili au tope. Uache kumuuza bilioni na ushee umpige benchi mchezaji msimu mzima huku unamlipa mchezaji mshahara na marupurupu kila mwezi halafu anaondoka bure kabisa.
 
Mbadala wa Messi pale Barca wamempata nani ?

Hivi Messi kauzwa au kamaliza mkataba wake ?

Leo Magazeti Yameandika Pogba Hauzwi Mwanaspoti Wakati Timu yakovya simba Inauza bila Kuwa na Mbadala....Jibu na Hili la Pogba
 

Hata Arsenal ilikuwa na Thienry henry,Robin van Persie,Marc Overmass,Nk Timu iko waoi sasa???
 
Kwahiyo hao watu walitakiwa wawepo Arsenal mpaka sasa ?

Watu wanaondoka Kwa Time Mkuu....
Ameshafanya Kile Club ilikuwa inahitaji na Mbadala wake amepatikana!
Sio Blaa blaa za Ooooh walikuwepo kina Flani hapa!
Ngoja Mtamjua Manara ni Nani Pale Simba Itakapokutana Na Yanga na Simba Akafungwa achilia mbali Kuchukua Vikombe[emoji3516][emoji30][emoji30]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…