Kwa mpira wa jana wa Tanzania sitaki kusikia tena dhihaka kwa Simba na story za papatupapatu

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Jana Tanzania imefuzu kwenda AFCON baada ya kutoka suluhu na Algeria.

Imekuwa ni desturi iliyojengeka mitandaoni na vyombo mbalimbali vya redio kuisema vibaya Simba hata pale inapopata matokeo yaliyo katika malengo ya timu. Hili halijaanza msimu huu tu, tukirudi hata msimu uliopita hizi fyokofyoko zilikuwa nyingi sana. Imefika hadi watagazaji wa mpira uwanjani nao wameingia katika huu ujinga.

Baada ya jana Tanzania kufuvu, kuna watu wanazunguka mitandaoni na kwenye vyombo vya habari wanasema tuliokuwa tunakosoa lolote kuhusu timu ya taifa tumeaibika. Wanasema hata kama umiliki mpira tulizidiwa kwa 80% kwa 19%, hata kama tulipiga pasi sahihi 65 dhidi ya 538 za kwao, hata kama usahihi wa pasi zetu ulikuwa ni 46% dhidi ya 88% zao wanatuambia muhimu mpira ni mbinu na malengo. Wanakopa maneno tuliyokuwa tunawaambia kitambo kuhusu Simba ila huko nyuma hawakutaka kusikia. Wanasema Simba anacheza mpira papatupapatu ila kwa mpira wa jana hilo neno ni haramu kutumika ingawa ukiwauliza maana ya papatupapatu ni nini wanakwambia ni kushindwa kucheza mpira wa pasi nyingi na kushindwa kutoa pasi za uhakika.



Leo hii wanamuimba na kumpamba Dennis Kibu kwa jinsi alivyocheza jana wakati ndiyo anavyochezaga kila siku pale Simba na kuna mechi kubwa za Simba amecheza vizuri zaidi ya alivyocheza jana ila hawajawahi kumkubali zaidi ya kumuongelea kwa dhihaka tu na dharau.

Siku nyingine tukiwaambia mpira ni malengo mkae kwa kutulia na mpunguze vidomodomo.
 
Huku ni ngazi ya Taifa mkuu,subiri Ligi ikianza tutaongea
 
Waaambie wale wanaotaka Pirra biriani lkn wakiwa wamepoteza mchezo ni Ujinga na Upuuzi. Simba alichukua Ngao ya Hisani kimbinu halafu kuna Vimbwengo wakawa wanabeza.
 
Uko wapi Mkuu, uje hapa Break Point ,Makumbusho upate hata Soda ,
 
Waaambie wale wanaotaka Pirra biriani lkn wakiwa wamepoteza mchezo ni Ujinga na Upuuzi. Simba alichukua Ngao ya Hisani kimbinu halafu kuna Vimbwengo wakawa wanabeza.
Tupo kwenye ligi kuu sasa hakuna penalty shootout bali ni mwendo wa kukusanya point nyingi na magoli mengi. Tuone timu ipi itafanikiwa kwa aina ya mchezo, mbinu na kikosi kilichonacho.
 
Wanaopiga kelele wengi ni nyie wenyewe mashabiki wa Simba kuwa huo sio mpira mliouzoea. Hamjazoea mpira presha kushikilia bomba, moyo na kubana mapumbu mda wote, hamjazoea kupelekewa moto muda wote bali nyie ndio wapelekaji pumzi ya moto kila muda. Hamjazoea mpira butua ilimradi uende, hamjazoea kuona timu inashindwa kupiga pasi hata kumi pasipo kupoteza mpira jambo ambalo hata wewe mwenyewe ulikuja kulisemea hapa kwa mazoezi ya Rondo.
 
Kwa hiyo tuhalalishe kwamba mashabiki wa Simba mnapenda pira PAPATUPAPATU?
Kesho msilalamike mkiitwa hivyo!
 
"papatupapatu"
Hii ndio kupapasa papasa?
Hilo ni pira ambalo wachezaji muda wote wanakimbia kimbia tu uwanjani kama nyumbu vile waliojeruhiwa na majangili!
Yaani timu inaweza ikashinda, lakini hata magoli hayaeleweki yameingiaje!! Hilo pira linachezwa kwa sasa na timu fulani hivi.
 
Hilo ni pira ambalo wachezaji muda wote wanakimbia kimbia tu uwanjani kama nyumbu vile waliojeruhiwa na majangili!
Yaani timu inaweza ikashinda, lakini hata magoli hayaeleweki yameingiaje!! Hilo pira linachezwa kwa sasa na timu fulani hivi.
Hahahaaaa.... Nacheka kama mazuri lakini bado tunasafari ndefu ya kuujua mpira wetu.

Yaani mnataka timu zicheze staili ya kufanana wakati zinamakocha wawili tofauti wenye falsafa mbili tofauti kabisa, jambo ambalo haliwezekani.

Ko msifosi zifanane kila mtu apambane na timu lake.
 
Mimi nimetoa tu maana halisi ya pira papatu papatu. Na pia nimetolea mfano wa timu inayocheza aina hiyo ya mpira. Hakuna sehemu nimesema timu zote zicheze mpira unaofanana.
 
Mimi nimetoa tu maana halisi ya pira papatu papatu. Na pia nimetolea mfano wa timu inayocheza aina hiyo ya mpira. Hakuna sehemu nimesema timu zote zicheze mpira unaofanana.
Kila mtu apambane na timu lake tutaona mwisho wa hizi marathon.....

Sasa mnang'ang'ana kuonyesha mapungufu ya Simba ikiimarika kama mnavyotaka mtaanza kuumia wenyewe tena....
 
Jana nilishindwa kushangaa, yaan Algeria pira lote lile eti shoot on target tumelingana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…