SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Jana Tanzania imefuzu kwenda AFCON baada ya kutoka suluhu na Algeria.
Imekuwa ni desturi iliyojengeka mitandaoni na vyombo mbalimbali vya redio kuisema vibaya Simba hata pale inapopata matokeo yaliyo katika malengo ya timu. Hili halijaanza msimu huu tu, tukirudi hata msimu uliopita hizi fyokofyoko zilikuwa nyingi sana. Imefika hadi watagazaji wa mpira uwanjani nao wameingia katika huu ujinga.
Baada ya jana Tanzania kufuvu, kuna watu wanazunguka mitandaoni na kwenye vyombo vya habari wanasema tuliokuwa tunakosoa lolote kuhusu timu ya taifa tumeaibika. Wanasema hata kama umiliki mpira tulizidiwa kwa 80% kwa 19%, hata kama tulipiga pasi sahihi 65 dhidi ya 538 za kwao, hata kama usahihi wa pasi zetu ulikuwa ni 46% dhidi ya 88% zao wanatuambia muhimu mpira ni mbinu na malengo. Wanakopa maneno tuliyokuwa tunawaambia kitambo kuhusu Simba ila huko nyuma hawakutaka kusikia. Wanasema Simba anacheza mpira papatupapatu ila kwa mpira wa jana hilo neno ni haramu kutumika ingawa ukiwauliza maana ya papatupapatu ni nini wanakwambia ni kushindwa kucheza mpira wa pasi nyingi na kushindwa kutoa pasi za uhakika.
Leo hii wanamuimba na kumpamba Dennis Kibu kwa jinsi alivyocheza jana wakati ndiyo anavyochezaga kila siku pale Simba na kuna mechi kubwa za Simba amecheza vizuri zaidi ya alivyocheza jana ila hawajawahi kumkubali zaidi ya kumuongelea kwa dhihaka tu na dharau.
Siku nyingine tukiwaambia mpira ni malengo mkae kwa kutulia na mpunguze vidomodomo.

Ukiwa na possesion kubwa sana lakini usifanikiwe kupata goli hiyo siyo crediti kwako!! Maana yake ni kwamba hukujua uufanyie nini mpira wakati unakaa nao!! Ukiwa na possesion kidogo sana lakini haukuruhusu goli maana yake ni kwamba unajua kucheza vizuri wakati ukiwa hauna mpira!! hivyo kumnyima kabisa nafasi aliye nao mpira kuufanyia kitu cha maana, hiyo ni CREDIT kubwa sana!!
Kwenye mpira wa kisasa unatakiwa ujue jinsi ya kucheza wakati ukiwa na mpira na wakati ukiwa huna mpira!! Taifa stars ni mashujaa sana.