General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,064
Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?
Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake
Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.
Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.
Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.
Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.
Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam
Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.
Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.