kama ni tanker la mafuta yanakuwaga na lita 30,000-35,000,jamaa akishapanga kuwa leo naliangusha iwe isiwe,,basi akishaendambali sana,pengine mafuta yanaenda songea na anajua tajiri yupo dar,,anahakikisha lzm afike njombe au makambako usiku mkubwa,na akifika tu wese linamiminwa kwenye kisima cha sheli km lita 20,000,na huo mpango unakuwaga ushachongwa mapema kati ya dereva na tajiri wa sheli,km tajiri ananunua lita1 hadi kufikisha makambako labda ni 1800-basi hapo dereva anamletea hadi kituoni kwa 1200 mara lita 20,000 dereva anakomba milioni zake 24 safi,kisha taratibu saa kumi afajir anaanza kuondoka makambako akitafuta yale makona kona mengi pale mlimani mwanaume analilaza kiheshima mahali kisha analegeza vifuniko wese lililobaki liendelee kumwagika chini taratibu kabla wachomoa betri hawajafika kulimalizia wese lote,,ila miaka ya sasa naona hayo madili yamepungua maana matajiri wengi wanafunga ma camera na GPS,wanakusoma tu ukiwa njiani na unachokifanya,,,,kuna mmoja miaka ya 2004 alikua na lori lake limekula kinywaji ya TBL full,akafika njiani akauza kama nusu ya mzigo,alikua anatoka arusha kwenda singida,,wanadai mzigo aliuzia babati na lipofika maeneo ya sigino kwenye mlima logia akajidai limemshinda,akaruka lori likatumbukia shimoni,,ile kinywaji ya TBL ilobakia kwenye gari wanakijiji wa pale sigino walilewa kijiji kizima,,hata wale wasiokunywaga siku hiyo walitest kinywaj pendwa na wakalewa chakari,,ogopa hadi watoto na wamama walilewa,maana vijana na wababa walikua wanaenda eneo la ajali wanabeba makreti na kuyakimbiza kijijini majumbani kwao kisha wanarudi kuchukua tena,,wakati huo kule home watoto wanafungua chupa na kutest wakijua ni soda