Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

200k kwenda chini hukatwi kodi nadhan

Hata hivyo kweli matajiri wa bongo wanyonyaji wanalipa kiduchu sana tofauti na matajiri wa nchi zingne
Mwisho wa Tax Free ni 170,000/-. Above hapo kodi itahusika tu.
 
Kuna mtu akiwanyoosha hawa mnasema anawachukia. Acheni tu wasiingiliwe maanake watafunga biashara halafu mtoe lawama mtetezi wa wanyonge anaua uchumi.

Mtu yeyote mwenye uchungu na nchi ukiingia deep na kuwajua vizuri hawa 'matajiri' ukipata nafasi lazima uwanyooshe
Kunyoosha kupi unakosema wewe? Au ni kule kwa kubambikia watu kesi sawa na wengine wanavyonyooshwa kwa kutekwa na kupotezwa? Acheni kuhalalisha ushenzi na udhalimu kwa sababu yoyote ile. Kama kweli huyo mtu wenu ana huo uchungu unaotaka kudanganya watu kwamba anao, aanze kwanza kupandisha kima cha chini serikalini! Ana mwaka wa 3 madarakani, je amefanya hivyo?! Mfano mwingine mdogo kabisa, kwa mujibu wa sheria, mwajiri yeyote mwenye wafanyakazi 100+ anatakiwa kuajiri angalau 3% walemavu! Je, unataka kutuambia serikali imefikisha hiyo idadi?!

Endeleeni kuhalalisha ushenzi na ufedhuli mkidhani na wenyewe mpo salama!! NI ujinga kudhani unaweza kufanya maisha ya Watanzania maskini kuwa mazuri kwa kuwafanyia ufedhuli walionacho kama walivyofanya kwa Yusufu Manji! Now tell me, mtu kama Yusuf walimsakizia kesi ya dawa za kulevya, uhujumu uchumu pamoja na kuhatarisha usalama wa taifa! Baada ya hayo, mfuko wako uliongeza shilingi ngapi za mapato zilizotokana na huo ufedhuli wenu unaoushabikia?
 
Sikuiona hii post mkuu...

Hata hivyo, uliandika vitu ambavyo havihusiani, Kwa mfano unauliza jarida la Forbes wanatumia vigezo gani kujua utajiri wa mtu bila kuangalia hali za wafanyakazi wake?! Hakuna uhusiano hapa, Tena unasema unamlipaje mtu pesa kidogo ili hali ana majukumu ya kusomesha, umeme na maji et cetera, niseme hivi, malipo ya mtu hayategemei majukumu aliyonayo, inategemea productivity yake, kiwango cha elimu yake, nafasi ya kazi aliyonayo na vitu vingine..

Naomba "kutangaza" interest(nimesahau spelling za kudikrea) MO is among my role models, lakini simtetei alipe wafanyakazi mishahara midogo na wala sijui kima cha chini wala cha juu cha mshahara ni kipi, nilitaka kuonyesha vitu ulivyoandika, ambavyo havina uhusiano.
 
bonas mkuu hazitambuliki kisheria, zinaweza kuwepo au zisiwepo.

Mshahara gani upo chini ya kima cha chini kwa kampuni ya Tajiri namba moja?

Huu ni unyonyaji mtupu.
I agree, waulize bunge kilichowapata
 
Anafaidika vipi akilipigisha gari mzinga?
Nadhani hapa alimaanisha Baadhi ya Madereva wasio waaminifu huuza mali (Mf. Mafuta) kuchikichia pesa na kubakiza mali kiasi ili akiangusha gari porini imwagike kupoteza ushahidi wa dili alilofanya.
 
Ni kweli . Kwa hili namsifu sana Bakhresa kwa kujali wafanyayakazi wake.
 
Kumbuka angeweza kufanya kazi zote asingetoa ajira kwa yeyote. Hivyo ukiona akufanyii poa fanya kazi za kwako kulingana na fursa ulizonazo.
 
shida wafanyakazi wengi hawajitambui.. kazi ya mshahara laki na 30 unaandika barua ya kuiomba ya nini?

mfumo wetu wa elimu na maisha ni mbovu.. kuna graduates wengi sana wamefanya kazi hata 10 yrs wengine ila hana asset yeyote zaidi ya liabilities kibao... akiachishwa kazi umwambie atafute hata laki 3 kwa mwezi sawa na elfu 10 kila siku hawezi... mtu kama huyu kazi hata ya laki moja anaandika barua anaomba..

hivi dereva ulipwe laki moja.. huwezi hata kuuza chips, maji, mtaani
Usiombe wanaohitaji wataomba.
Confess.
Niliajiliwa mwaka 93 gross salary na marupurupu 13500 kwa hao wahindi.
Sikusaini mkataba ile naondoka rafiki yangu alikua kazini pale kipindi akaniona. Kuniuliza vp.
Nikamweleza mi nilikua interview jamaa hela ni hii wanatoa, hela hii mi naipata kwa wiki nikipiga mishe.
Jamaa akanambia acha umbwela ww kasaini mkataba kisha tutakuonyesha.
Na kweli baada ya hapo nilikua natimua na kimshahara daily nyumbani×30=¿+13500,life was good

Unajiongeza tu.
 
Eeegh..., halafu kumbe ni gross, maana yake net inaweza ikawa 20,000/= tu, wanategemea huyo mtu anaishije Dar hapa?
 
Kibao kimegeuka duh!
There is a thin line between love and hate walahi
 
Kunyoosha kupi unakosema wewe? Au ni kule kwa kubambikia watu kesi sawa na wengine wanavyonyooshwa kwa kutekwa na kupotezwa? Acheni kuhalalisha ushenzi na udhalimu kwa sababu yoyote ile. Kama kweli huyo mtu wenu ana huo uchungu unaotaka kudanganya watu kwamba anao, aanze kwanza kupandisha kima cha chini serikalini! Ana mwaka wa 3 madarakani, je amefanya hivyo?! Mfano mwingine mdogo kabisa, kwa mujibu wa sheria, mwajiri yeyote mwenye wafanyakazi 100+ anatakiwa kuajiri angalau 3% walemavu! Je, unataka kutuambia serikali imefikisha hiyo idadi?!

Endeleeni kuhalalisha ushenzi na ufedhuli mkidhani na wenyewe mpo salama!! NI ujinga kudhani unaweza kufanya maisha ya Watanzania maskini kuwa mazuri kwa kuwafanyia ufedhuli walionacho kama walivyofanya kwa Yusufu Manji! Now tell me, mtu kama Yusuf walimsakizia kesi ya dawa za kulevya, uhujumu uchumu pamoja na kuhatarisha usalama wa taifa! Baada ya hayo, mfuko wako uliongeza shilingi ngapi za mapato zilizotokana na huo ufedhuli wenu unaoushabikia?
E19A8184-CE01-470B-BBA9-F41B964A76E4.jpeg
 
Kuna mtu akiwanyoosha hawa mnasema anawachukia. Acheni tu wasiingiliwe maanake watafunga biashara halafu mtoe lawama mtetezi wa wanyonge anaua uchumi.

Mtu yeyote mwenye uchungu na nchi ukiingia deep na kuwajua vizuri hawa 'matajiri' ukipata nafasi lazima uwanyooshe
Mtumeee
 
Sio huyu tu mbona wako wengi sana .Ila kwa muindi hizo ndio range zao
 
Hivi una habari kwamba hakuna mtu niliyemdharau humu jamvini kama wewe? Sijawahi kukuona ukitoa hoja zaidi ya kubisha kila kitu kama ambavyo bila aibu majuzi ulibisha suala la kutekwa Mo Dewji na kwa aibu ile ile uka-delete post! Hata kama ni ushabiki wa kisiasa, wa kwako unakufanya uonekane completely dumb!
 
Back
Top Bottom