Kunyoosha kupi unakosema wewe? Au ni kule kwa kubambikia watu kesi sawa na wengine wanavyonyooshwa kwa kutekwa na kupotezwa? Acheni kuhalalisha ushenzi na udhalimu kwa sababu yoyote ile. Kama kweli huyo mtu wenu ana huo uchungu unaotaka kudanganya watu kwamba anao, aanze kwanza kupandisha kima cha chini serikalini! Ana mwaka wa 3 madarakani, je amefanya hivyo?! Mfano mwingine mdogo kabisa, kwa mujibu wa sheria, mwajiri yeyote mwenye wafanyakazi 100+ anatakiwa kuajiri angalau 3% walemavu! Je, unataka kutuambia serikali imefikisha hiyo idadi?!
Endeleeni kuhalalisha ushenzi na ufedhuli mkidhani na wenyewe mpo salama!! NI ujinga kudhani unaweza kufanya maisha ya Watanzania maskini kuwa mazuri kwa kuwafanyia ufedhuli walionacho kama walivyofanya kwa Yusufu Manji! Now tell me, mtu kama Yusuf walimsakizia kesi ya dawa za kulevya, uhujumu uchumu pamoja na kuhatarisha usalama wa taifa! Baada ya hayo, mfuko wako uliongeza shilingi ngapi za mapato zilizotokana na huo ufedhuli wenu unaoushabikia?