Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

mshahara 130,000
wafanyakazi 24,000

kweli mshahara ni mdogo sana .
 
Aisee! Kumbe bora nikomae na forex ambayo nikiwa na mtaji wa dola 100 naweza kutengeneza faida ya dola 500 kwa mwezi!

Kumbe kuna watu wanapata kamshahara kiduchu hivi?
 
Kuna mtu akiwanyoosha hawa mnasema anawachukia. Acheni tu wasiingiliwe maanake watafunga biashara halafu mtoe lawama mtetezi wa wanyonge anaua uchumi.

Mtu yeyote mwenye uchungu na nchi ukiingia deep na kuwajua vizuri hawa 'matajiri' ukipata nafasi lazima uwanyooshe
Mkuu kila ninaposoma comment zako, naona ni MTU Mwenye busara Sana.
 
Kibarua wangu (saidia Fundi ) namlipa 15000 kwa Siku. Lkn the same person akifanya kazi hiyo kwenye makampuni ya kichina au makampuni makubwa ya ujenzi analipwa 7000 -10000 kwa siku.
 
Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?

Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake

Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.

Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.

Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.

Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.

Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam

Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.

Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.

View attachment 718025View attachment 718026

Mkuu acha uvivu fanya research kabla ya kutujazia server, kuna bonasi, overtime, na kidebe (mipigo) waliowahi kufanya kazi Kwa wahindi kama Pepsi wanaelewa hii kitu, usishangae unaowasemea wanalipwa kiduchu wanaishi Maisha mazuri kuliko unayepiga porojo
 
Ndio maana wizi nchi hii hauishii, huwezi kumlipa mtu 130k ukitarajia ufanisi na uaminifu kazini.
 
Kuna mtu akiwanyoosha hawa mnasema anawachukia. Acheni tu wasiingiliwe maanake watafunga biashara halafu mtoe lawama mtetezi wa wanyonge anaua uchumi.

Mtu yeyote mwenye uchungu na nchi ukiingia deep na kuwajua vizuri hawa 'matajiri' ukipata nafasi lazima uwanyooshe
Unawanyoosha kupitia sheria siyo kimafia, vinginevyo utapalilia vita vya wenyewe kwa wenyewew, hata hicho ulidhamiria huta kipata
 
Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?

Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake

Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.

Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.

Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.

Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.

Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam

Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.

Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.

View attachment 718025View attachment 718026
Tatizo ni Sera mbovu za chama tawala ambazo zinapelekea sheria mbovu ambazo. Bdo hizo sheria mbovu hazitekelezwi kikamilifu.

Kama mshahara waTshs. 130,000 ni kinyume na sheria yu wapi waziri wa kazi na ajira??
 
Unyonyaji ni ngumu kuisha,siyo Mo tu pitia kampuni za kichina utashangaa
 
...acha kazi huone kazi,huh ni msemo ya kijinga sana wengi unawafanya wawe watumwa WA kazi,...
Fanya kazi upate uzoefu wa hyo kazi instead ya pesa...
Uvivu na ujinga ndo unatufanya tuwe hivyo..
 
Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.

Kweli Mkuu, tena hiyo Tshs 130,000 ni gross ikimaanisha ina makato.

Lakini labda tuanzie upande wa srikali. Hivi mshahara kima cha chini ni Tshs ngapi? Maana kama wanadiriki kutangaza mshahara hadharani ulio chini ya kiwango cha serikali cha kima cha chini wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Je, serikali ya Magufuli imechukua hatua gani kuhakikisha sekta zote chini zinalipa wafanyakazi kulingana na sera ya serikali ya mshahara wa kima cha chini?

Kimsingi, hata ukiwa na housegirl kwenye nyumba yako unapaswa kumlipa mshahara kima cha chini kwa kiwango cha chini kabisa. Sasa unaweza kurekebisha kulingana na huduma unazompa, kama mavazi, matibabu nk.

NB. Nasoma kwamba kima cha chini kilichowekwa na serikali ni Tshs 300,000. Kwa mantiki hiyo basi, wa kulaumiwa ni serikali ya Magufuli kushindwa kusimamia haki za Watanzania kulipwa kulikana na sheria za nchi, na waajiri kwa kiburi kabisa kutangaza mishahara hadharani inayopingana na kima cha chini cha serikali.
 
Matajiri waliowengi ni wachoyo hawapendi wenzao watajirike,tabu za wengine ni furaha kwa tajiri.
 
i
Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?

Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake

Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.

Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.

Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.

Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.

Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam

Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.

Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.

View attachment 718025View attachment 718026
takuwa ni mshahara kwa wiki labda,,kwa mwezi haiwezekani,,,ntauza bidhaa zote na gari nauza pia nasepa zangu mtukula kufungua kiosk
 
Sasa hata ungekuwa wewe tajiri sidhani kama ungekuwa unamlipa dereva laki 5 au laki 7....tuangalie gharama za uendeshaji kampuni, gharama ya kodi, gharama ya magari n.k . Na hapo ni mshahara wa mwanzo wa dereva, hivi tuseme ukweli bora usiwe na kazai mtaani au bora ufanye kazi hiyo ya 130k. Ajira ngumu jamani, nigeria wasomi kibao wanaosha magari, mbona wabongo tunakimbilia mshahara mkubwa hata kabala hujaanza kazi? Mshahara unaanzia hapo ila nina imani kadri unavyoendelea ndipo mshahara utapanda. Tusilaumu sana matajiri, kiukwel hawa matajiri wamesaidia sana jamii, kwa hiyo hiyo 130k mtu anakula na anasomesha fresh. Na watu mngekuwa matajiri hata hiyo 130k msingetoa mngetoa chini zaidi ya hapo
 
Anafaidika vipi akilipigisha gari mzinga?
kama ni tanker la mafuta yanakuwaga na lita 30,000-35,000,jamaa akishapanga kuwa leo naliangusha iwe isiwe,,basi akishaendambali sana,pengine mafuta yanaenda songea na anajua tajiri yupo dar,,anahakikisha lzm afike njombe au makambako usiku mkubwa,na akifika tu wese linamiminwa kwenye kisima cha sheli km lita 20,000,na huo mpango unakuwaga ushachongwa mapema kati ya dereva na tajiri wa sheli,km tajiri ananunua lita1 hadi kufikisha makambako labda ni 1800-basi hapo dereva anamletea hadi kituoni kwa 1200 mara lita 20,000 dereva anakomba milioni zake 24 safi,kisha taratibu saa kumi afajir anaanza kuondoka makambako akitafuta yale makona kona mengi pale mlimani mwanaume analilaza kiheshima mahali kisha analegeza vifuniko wese lililobaki liendelee kumwagika chini taratibu kabla wachomoa betri hawajafika kulimalizia wese lote,,ila miaka ya sasa naona hayo madili yamepungua maana matajiri wengi wanafunga ma camera na GPS,wanakusoma tu ukiwa njiani na unachokifanya,,,,kuna mmoja miaka ya 2004 alikua na lori lake limekula kinywaji ya TBL full,akafika njiani akauza kama nusu ya mzigo,alikua anatoka arusha kwenda singida,,wanadai mzigo aliuzia babati na lipofika maeneo ya sigino kwenye mlima logia akajidai limemshinda,akaruka lori likatumbukia shimoni,,ile kinywaji ya TBL ilobakia kwenye gari wanakijiji wa pale sigino walilewa kijiji kizima,,hata wale wasiokunywaga siku hiyo walitest kinywaj pendwa na wakalewa chakari,,ogopa hadi watoto na wamama walilewa,maana vijana na wababa walikua wanaenda eneo la ajali wanabeba makreti na kuyakimbiza kijijini majumbani kwao kisha wanarudi kuchukua tena,,wakati huo kule home watoto wanafungua chupa na kutest wakijua ni soda
 
Back
Top Bottom