Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtanzania kadri unavyomlipa mshahara mkubwa ndio anazidi kuwa mvivu.......Sasa unamlipa mtu 130,000/= hiyo motisha ya kufanya kazi anaitoa wapi?
Anafanya tu bora liende ila ukimlipa vizuri na kuset rules zako kazi zinafanyika vizuri tu.
Umeona point mkuu.Mkuu naomba nifafanue hapa kuhusu hicho Kidogo wanachopata. Hii nafasi ya hawa SalesPerson cum driver, wanapewa Allowance ya Tsh. 100 katika Kila Carton 1 ya Maji au Soda. Akiuza Carton 100 kwa siku Ana Tsh. 10,000/= x siku 26 ni 260,000/= kwa mwezi, wakati mwingine hata Jumapili wanaingia kazini. Hapo ni kama Ameuza Cartons 100, wapo ambao wanauza mpaka cartons 500 per day. Ukiangalia huu mfumo ndo wenzetu wa Nchi zilizoendelea wanatumia, yani mtu alipwe kulingana na alichozalisha. Utaona kwa sisi ambao tunapenda Kazi ya Sales, hatuangalii Mshahara, Tunaangalia percentage on Commission based. Ugonjwa mkubwa wa Watanzania waliyo wengi anataka aone fixed salary ili apate mtelemko kila mwisho wa mwezi. Yani ufanye kazi usifanye mwisho wa mwezi hela yako iingie. Huu Upuuzi ambao matajiri wengi walishaachana nao. Hata ningekua ni Mimi lazima nione unachozalisha katika kampuni ndo nikupe mshahara mzuri. Watanzania Tubadilike. Vijana wengo mnaotoka chuoni mkiambiwa njoo ufanye kazi ya Commission hamtaki kwasababu mnapenda mitelemko. Dunia imebadilika. Mwisho, Hiyo 130,000/= wanalipwa kama hela ya Kujikimu tu In case hajafanya mauzo mwezi mzima, lakini kinyume chake Commission wanazopata ni kubwa maradufu kuliko mshahara ambao ww umelalamikia hapa. Asante
Mleta uzi alicho shauri ni hiki; serikali isiwe busy tu na Mange Kimambi, ikomae na wafanya baishara wasio fata sheria, kima cha chini cha mshahara Tanzania kinajulikana.Katika mfumo wa kibepari mfanyakazi ni gharama tu anaepunguza faida hivyo....the lower the cost the better...kwa maana nyingine lengo lake ni kuwa na gharama ndogo iwezekanavyo.....uhuru wa kweli ninkujiamini na kutafuta fursa inayoendana na thamani yako...
Hapo unakosea mkuu. Tupo ambao sio wavivu wala wazembe.Mtanzania kadri unavyomlipa mshahara mkubwa ndio anazidi kuwa mvivu.......
Mshahara haumpi Mtanzania motisha ya kazi bali unampa nafasi ya kuwa mzembe na mwenye kiburi kazini....
Naongea kutokana na uzoefu
Mkuu ,wewe unawashangaa hao tu?Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?
Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake
Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.
Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.
Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.
Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.
Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam
Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.
Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.
View attachment 718025View attachment 718026
Mkuu mi naamini wewe ni member wa muda mrefu humu unajua kutofautisha baina ya kitu official na habari ambayo haijathibitishwa.Huwa najiuliza sana taasisi kama Forbes inatumia vigezo gani kumjua tajiri namba moja katika nchi husika. Wanashindwa hata kutembelea wafanyakazi wa kampuni za tajiri husika kuangalia hali zao nao zikoje?
Juzi hapa nilileta bandiko kuhusu mishahara ya wafanyakazi wanaofanya katika kampuni za matajiri hawa wawili hapa Tz, Mo Dewji na Bakhresa.
METL GROUP, BAKHRESA GROUP Kampuni kubwa Tanzania zisizojali Wafanyakazi wake
Nilieleza jinsi wanafunzi wa nchi kama Marekani, hata hapo Kenya wanavyotamani kufanya kazi katika kampuni za matajiri wa nchi zao.
Lakini kwa hapa Bongo mambo ni tofauti kabisa, wafanyakazi wa Mo na Bakhersa wanafanya kazi kwakua hakuna mbadala, ajira hakuna. Na hiki ndicho kigezo hutumia kuwanyonya wafanyakazi kwani wanajua hana pa kwenda hata kama mshahara ni mdogo.
Embu wana JF tuangalie hili tangazo la kampuni ya tajiri namba moja Tz, Dewji.
Ni la dereva atakae husika na mauzo pia.
Hivi kweli kwa hali ya hapa Dar unamlipaje mtu mshahara wa Tsh 130,000 kwa mwezi? Mtu huyo anafamilia, analipa kodi, anasomesha, umeme, maji nk Ushahidi link hii hapa chini na screenshot zake, wasije wakabadilisha au kulitoa.
Salesperson Cum Driver. in Dar Es Salaam
Yani hata kima cha chini hawaja kifikia. Mbaya zaidi Serikali inajua haya lakini wanashindana na Mange Kimambi mitandaoni.
Waziri wa kazi na ajira tekeleza majukumu yako, sioni sababu ya nyie kushikilia nafasi hizo huku wananchi wanabyonywa na hawa mabepari wanao zidisha umasikini kwa wananchi.
View attachment 718025View attachment 718026
hicho wanachokifanya ni ukwepaji wa kodi.This is what you can see from outside....mara kadhaa kuna incentives zimefichwa....
Nimewahi kufanya kazi Quality Group.....nliona payslip ya Financial Controller, an expat from India akilipwa laki 5 back in mid 2000....nikashangaa sana...
later on nikaja kufahamu kumbe kulikuwa na payroll mbili....hiyo ya laki 5 ambamo kuna statutory deductions kama Pension contributions na PAYE na payroll nyingine ya siri isiyo na deductions zozote....
Mkuu nakuambia tena: hakuna tajiri asiyedhulumu.sio wote rudisha maneno yako mdomoni, unamkosea hata mungu.