Mkuu naomba nifafanue hapa kuhusu hicho Kidogo wanachopata. Hii nafasi ya hawa SalesPerson cum driver, wanapewa Allowance ya Tsh. 100 katika Kila Carton 1 ya Maji au Soda. Akiuza Carton 100 kwa siku Ana Tsh. 10,000/= x siku 26 ni 260,000/= kwa mwezi, wakati mwingine hata Jumapili wanaingia kazini. Hapo ni kama Ameuza Cartons 100, wapo ambao wanauza mpaka cartons 500 per day. Ukiangalia huu mfumo ndo wenzetu wa Nchi zilizoendelea wanatumia, yani mtu alipwe kulingana na alichozalisha. Utaona kwa sisi ambao tunapenda Kazi ya Sales, hatuangalii Mshahara, Tunaangalia percentage on Commission based. Ugonjwa mkubwa wa Watanzania waliyo wengi anataka aone fixed salary ili apate mtelemko kila mwisho wa mwezi. Yani ufanye kazi usifanye mwisho wa mwezi hela yako iingie. Huu Upuuzi ambao matajiri wengi walishaachana nao. Hata ningekua ni Mimi lazima nione unachozalisha katika kampuni ndo nikupe mshahara mzuri. Watanzania Tubadilike. Vijana wengo mnaotoka chuoni mkiambiwa njoo ufanye kazi ya Commission hamtaki kwasababu mnapenda mitelemko. Dunia imebadilika. Mwisho, Hiyo 130,000/= wanalipwa kama hela ya Kujikimu tu In case hajafanya mauzo mwezi mzima, lakini kinyume chake Commission wanazopata ni kubwa maradufu kuliko mshahara ambao ww umelalamikia hapa. Asante