bonas mkuu hazitambuliki kisheria, zinaweza kuwepo au zisiwepo.
Mshahara gani upo chini ya kima cha chini kwa kampuni ya Tajiri namba moja?
Huu ni unyonyaji mtupu.
Mm siwezi kuwalaumu hata kidogo ila nalaumu mfumo uliowekwa na serikali kwa sbb kwa mfumo wao mbovu umesababisha kutokea kwa unemployment na kuwepo kwa sheria mbovu za malipo ya wafanyakazi.
*Sheria mbovu
-Hakuna sheria na km ipo ni dhaifu ya usimamizi wa malipo ya mfanyakazi na kibarua. Mfanyakazi anatakiwa alipwe shilingi ngapi kwa mwezi na kibarua kwa siku alipwe shilingi ngapi. Km serikali ilitakiwa waweke kiasi kwa mfano. Kibarua ni shilingi 15,0000 kwa siku kuanzia saa 2 asubuhi mpaka 12:00 jioni.
Lkn hapa wameachiwa wenye biashara na serikali imebaki kusimamia kwenye mikataba tu. Wao wakija wanataka wafanyakazi wawe wamesaini mkataba wa ajira/kazi lkn usimamizi wa malipo hakuna, Kutokana na sheria hizi mbovu tunapata fao la kujitoa ili upate hela uwe na miaka 55.
Unafikiri wafanyakazi wanaweza kupinga malipo madogo ikiwa kuna lindi la umasikini na ukosefu wa ajira? Jibu: No. Mfano mzuri tunaona serikali ikifuta ajira za walimu wa arts na NIDA. Unafikiri hawa watu wafanye kazi gani? Jibu: watalazimika wafanye kazi yyte ile ili mradi mkono uende kinywani. Kule mbweni kuna mhindi anawalipa watu 6,000 kuanzia saa 2 asb-12jioni. Unafikiri kwa usawa huu wa vyuma kukaza unafikiri mtu afanyaje?
*Unemployment.
Hili ndilo gonjwa kubwa linalotutesa watu wengi. Kila kukicha hakuna mikakati thabiti ya kupunguzz unemployment rate in TZ. Viongozi wanaishia kusema jiajirini vijana lkn wao wameajiajiriwa na wakistaafu wanapeana kazi mfano mzuri ni Benjamini, Kikwete na Pinda. Unategemea mm km kijana nifanye nn? Angalia masharti ya mkopo bank au taasisi zingine za fedha. Je, zipo sawa? Mm ambaye sina mali yyte yaan jinsi nilivyo je, naweza kukopa? Jibu hapana lazima uwe na mali utakayoiweka ili kukuwezesha kuchukua mkopo.
N.B
Mfumo wetu mbovu ndiyo umetufikisha hapa. Malipo ya ajira mara nyingi yanategemea sana unemployment rate na kiwango cha umasikini.
Mfano. Nyanya kwa ndoo ni 30,000 lkn wote mkilima nyanya na mkavuna ndoo inaweza shuka ikawa 3,000. Kila siku idadi ya watu wanaoanza maisha inaongezeka huku ajira hakuna kwahiyo mtu anaamua afanye kazi yyte ile ili mradi mkono uende kinywani.
Chukua mfano huu. Kwenye ujenzi (malipo ya siku) fundi huwa 30,000 au 25,000 na msaidizi ni 15,000. Hii ni bei inayojulikana. Sasa fanya hivi.
Kwa siku fundi ni 15,000 na msaidizi ni 8,000 uone km raia hawatafanya kazi. Maisha magumu watu wanaunga unga