Kwa mshahara huu, Mo Dewji utajiri wako unatokana na unyonyaji wa wafanyakazi wako

Kwani hakuna mamlaka ya serikali inayohusika na udhibiti wa viwango vya mishahara?
 
Mo Kweli NYOSO,Kuna Jamaa Shamba Boy Kazi Yake Kuu ni Kuhudumia Mifugo kuwapa Chakula (Kuku+Mbuzi na ChairFire) analipwa Laki na nusu.
Hahaha. Jamaa mpigaji mie kuna jamaa ninafahamu anafanya kazi ya kuhudumia kuku tu kwa mwezi anapata laki 1 na bado ana pata maji na umeme wa solar wa bure. Pasipo kusahau na eneo la kujilimia mboga mboga zake
 
shida wafanyakazi wengi hawajitambui.. kazi ya mshahara laki na 30 unaandika barua ya kuiomba ya nini?

mfumo wetu wa elimu na maisha ni mbovu.. kuna graduates wengi sana wamefanya kazi hata 10 yrs wengine ila hana asset yeyote zaidi ya liabilities kibao... akiachishwa kazi umwambie atafute hata laki 3 kwa mwezi sawa na elfu 10 kila siku hawezi... mtu kama huyu kazi hata ya laki moja anaandika barua anaomba..

hivi dereva ulipwe laki moja.. huwezi hata kuuza chips, maji, mtaani
Wanaoomba hizo kazi sio wote wanaangalia mshahara , wengine wanatafuta experience na kutengeneza CV tu
 
Ili uwe tajiri lazima uangalie namna ya KuCut Costs na KuMaximise profit.Hata kama ikibidi upate watu kukufanyia kazi bure!
 
Mkuu naomba nifafanue hapa kuhusu hicho Kidogo wanachopata. Hii nafasi ya hawa SalesPerson cum driver, wanapewa Allowance ya Tsh. 100 katika Kila Carton 1 ya Maji au Soda. Akiuza Carton 100 kwa siku Ana Tsh. 10,000/= x siku 26 ni 260,000/= kwa mwezi, wakati mwingine hata Jumapili wanaingia kazini. Hapo ni kama Ameuza Cartons 100, wapo ambao wanauza mpaka cartons 500 per day. Ukiangalia huu mfumo ndo wenzetu wa Nchi zilizoendelea wanatumia, yani mtu alipwe kulingana na alichozalisha. Utaona kwa sisi ambao tunapenda Kazi ya Sales, hatuangalii Mshahara, Tunaangalia percentage on Commission based. Ugonjwa mkubwa wa Watanzania waliyo wengi anataka aone fixed salary ili apate mtelemko kila mwisho wa mwezi. Yani ufanye kazi usifanye mwisho wa mwezi hela yako iingie. Huu Upuuzi ambao matajiri wengi walishaachana nao. Hata ningekua ni Mimi lazima nione unachozalisha katika kampuni ndo nikupe mshahara mzuri. Watanzania Tubadilike. Vijana wengo mnaotoka chuoni mkiambiwa njoo ufanye kazi ya Commission hamtaki kwasababu mnapenda mitelemko. Dunia imebadilika. Mwisho, Hiyo 130,000/= wanalipwa kama hela ya Kujikimu tu In case hajafanya mauzo mwezi mzima, lakini kinyume chake Commission wanazopata ni kubwa maradufu kuliko mshahara ambao ww umelalamikia hapa. Asante
Kama unauhakika naulichokiandika basi nivizuri zaidi
 
Karibia Wahindi wote matajiri ni wanyonya Jason, wabaguzi. Nimefanya nao kazi nilishindwana nao. A learned person cannot work with them. Hawafai kwa ujumla
 
viwanda vingi Tanzania mishahara ni vichomi iwe unalipwa kwa siku,kwa wiki,kwa mwezi serikali imetutelekeza hizo ndo ajira!!Fanya uchunguzi viwandani utatamani ulie...!!
Ni Kweli kuna TAJIRI ana wiwanda vikubwa kibarua anamlipa Tsh 3000 kwa siku,mie nashangaa Waziri wa kazi/Ajira na Waziri wa Viwanda wapo tu kutwa kwenye Majukwaa kupiga bla bla za chama badala ya kwenda field kutetea maslahi ya wafanyakazi,hivi 3000 kwa siku inatosha?
 
Wauza maduka ya nguo kino wengi wanalipwa 150,000 leo kampuni kubwa inamlipa dereva 130,000!
Halafu Mawaziri wapo kazi Kuzunguka na VX tu kuhubiri ngonjera za sisiemu,Hawa wafanyabiashara type za Mo wabanwe,wanawanyonya wafanyakazi kupata faida kubwa kisha fedha wanaenda kujenga MIJUMBA UFUKWENI kisha hawakai watu au anakaa SHAMBA BOY tu na Kununua Migari ya Mabilioni kuyaanika Uwani halafu hawayaendeshi hislafu tu.
 
Kuna mtu akiwanyoosha hawa mnasema anawachukia. Acheni tu wasiingiliwe maanake watafunga biashara halafu mtoe lawama mtetezi wa wanyonge anaua uchumi.

Mtu yeyote mwenye uchungu na nchi ukiingia deep na kuwajua vizuri hawa 'matajiri' ukipata nafasi lazima uwanyooshe
Sio uwatengenezee mazingira mazuri ya biashara ili wawe wengi watengeneze ajira nyingi zenye staha
 
shida wafanyakazi wengi hawajitambui.. kazi ya mshahara laki na 30 unaandika barua ya kuiomba ya nini?

mfumo wetu wa elimu na maisha ni mbovu.. kuna graduates wengi sana wamefanya kazi hata 10 yrs wengine ila hana asset yeyote zaidi ya liabilities kibao... akiachishwa kazi umwambie atafute hata laki 3 kwa mwezi sawa na elfu 10 kila siku hawezi... mtu kama huyu kazi hata ya laki moja anaandika barua anaomba..

hivi dereva ulipwe laki moja.. huwezi hata kuuza chips, maji, mtaani
Wote tuliuza chipsi na mitumba mtaani itakuwaje kumbuka na kilimo cha tz kilivyo wengeni tumetumia gharama kulima tumepata mazao ya kutosha lakini bei ya mazao ni hasara
 
Mkuu naomba nifafanue hapa kuhusu hicho Kidogo wanachopata. Hii nafasi ya hawa SalesPerson cum driver, wanapewa Allowance ya Tsh. 100 katika Kila Carton 1 ya Maji au Soda. Akiuza Carton 100 kwa siku Ana Tsh. 10,000/= x siku 26 ni 260,000/= kwa mwezi, wakati mwingine hata Jumapili wanaingia kazini. Hapo ni kama Ameuza Cartons 100, wapo ambao wanauza mpaka cartons 500 per day. Ukiangalia huu mfumo ndo wenzetu wa Nchi zilizoendelea wanatumia, yani mtu alipwe kulingana na alichozalisha. Utaona kwa sisi ambao tunapenda Kazi ya Sales, hatuangalii Mshahara, Tunaangalia percentage on Commission based. Ugonjwa mkubwa wa Watanzania waliyo wengi anataka aone fixed salary ili apate mtelemko kila mwisho wa mwezi. Yani ufanye kazi usifanye mwisho wa mwezi hela yako iingie. Huu Upuuzi ambao matajiri wengi walishaachana nao. Hata ningekua ni Mimi lazima nione unachozalisha katika kampuni ndo nikupe mshahara mzuri. Watanzania Tubadilike. Vijana wengo mnaotoka chuoni mkiambiwa njoo ufanye kazi ya Commission hamtaki kwasababu mnapenda mitelemko. Dunia imebadilika. Mwisho, Hiyo 130,000/= wanalipwa kama hela ya Kujikimu tu In case hajafanya mauzo mwezi mzima, lakini kinyume chake Commission wanazopata ni kubwa maradufu kuliko mshahara ambao ww umelalamikia hapa. Asante
Naunga mkono hoja ndio maana ukienda ulaya tunafanya kazi kwa masaaa ili upate pesa tatizo sis tumeshalemaaa na ile ya mwisho wa mwezi ndio upate kingi ila matajiri hawawez kufanya hvyo

Ndio maana hata baa unalipwa kwa kreti ulizouza
 
Sijui kwa kweli mkuu ila kama ni kweli basi kuna namna.

Au kuna posho katikati ya mwezi, bima ya afya na benefits nyingine....
mkuu Hakuna Posho Kule Wala Bima Ya Afya Na Mikataba Ya Pale Ya Hovyo Kweli,mie Nimeshafanyakazi Pale Kwa Miaka 3 Sema Kilichokuwa Kinanisaidia Ni Wizi Kila Siku Nilikuwa Naiba Baada Ya Madili Yakuiba Kupotea Namie Kazi Nikaacha
 
Ni Kweli kuna TAJIRI ana wiwanda vikubwa kibarua anamlipa Tsh 3000 kwa siku,mie nashangaa Waziri wa kazi/Ajira na Waziri wa Viwanda wapo tu kutwa kwenye Majukwaa kupiga bla bla za chama badala ya kwenda field kutetea maslahi ya wafanyakazi,hivi 3000 kwa siku inatosha?
Shida Ya Serikali Ya Hapa Haina Kima Cha Chini Cha Mishahara Ya Wafanyakazi Wote Nchini Ndio Maana Unyonyaji Umekuwa Mwingi Na Serikali Inayajua Yote Hayo Mfano kwa hapa Tanzania viwanda vyote hapa nchini vinawalipa vibarua 3000 kwa masaa 12 Nambie Hapo Mtu Ana Survive Vipi Kwa Maisha Yasasa ?
 
Viongozi wetu hawatetei wala hawafatilii maslahi ya mfanyakazi,ukiona kiongozi anakimbizana na mfanyabiashara mara hivi mara hivi ujue anataka akatiwe fungu lake atulie basi.
 
Mkuu naomba nifafanue hapa kuhusu hicho Kidogo wanachopata. Hii nafasi ya hawa SalesPerson cum driver, wanapewa Allowance ya Tsh. 100 katika Kila Carton 1 ya Maji au Soda. Akiuza Carton 100 kwa siku Ana Tsh. 10,000/= x siku 26 ni 260,000/= kwa mwezi, wakati mwingine hata Jumapili wanaingia kazini. Hapo ni kama Ameuza Cartons 100, wapo ambao wanauza mpaka cartons 500 per day. Ukiangalia huu mfumo ndo wenzetu wa Nchi zilizoendelea wanatumia, yani mtu alipwe kulingana na alichozalisha. Utaona kwa sisi ambao tunapenda Kazi ya Sales, hatuangalii Mshahara, Tunaangalia percentage on Commission based. Ugonjwa mkubwa wa Watanzania waliyo wengi anataka aone fixed salary ili apate mtelemko kila mwisho wa mwezi. Yani ufanye kazi usifanye mwisho wa mwezi hela yako iingie. Huu Upuuzi ambao matajiri wengi walishaachana nao. Hata ningekua ni Mimi lazima nione unachozalisha katika kampuni ndo nikupe mshahara mzuri. Watanzania Tubadilike. Vijana wengo mnaotoka chuoni mkiambiwa njoo ufanye kazi ya Commission hamtaki kwasababu mnapenda mitelemko. Dunia imebadilika. Mwisho, Hiyo 130,000/= wanalipwa kama hela ya Kujikimu tu In case hajafanya mauzo mwezi mzima, lakini kinyume chake Commission wanazopata ni kubwa maradufu kuliko mshahara ambao ww umelalamikia hapa. Asante
Kwa hapo mi nimekuelewa mkuu,asante kwa ufafanuzi!!
 
Duh jamani hata mfanyakazi wa ndani anayelala na kula chakula anachokula bosi wake.. wala hapokei mshahara huo mdogo..

Na ile ya ujanja wa kupenya kwenye matundu ya sheria haikugusa nayo ina huhu..

Inasikitisha huyo tena na kazi ya udereva kwenda kulipwa kiasi hicho.. huku madereva wa watu binafsi wanaopata na mengi zaidi hadi lunch hawanunui wao kuanzia 350,000. Na wakifanya usiku au overtime pesa inaongezeka na Jumapili nayo mtu analipwa zaidi akihitajika.. kwa mwezi hata 500k mtu anabeba

Kwa mara ya kwanza nimesoma point toka kwako. Nimefurahi... Nitapata usingizi mzuri leo.
 
Back
Top Bottom