Ninasema hivi kwasababu ikitokea Simba ipoteze naona kutakuwa na mtifuano mkubwa sana ndani ya Klabu . Hasira kubwa ya Mashabiki itakuwa kwa uongozi mzima wa Simba.
Kwasasa Mashabiki wengi wa Simba walishatoa msimamo wao kuwa hakuna kupeleka timu , hivyo wameutega uongozi wa Simba. Ikitokea Simba ishinde litakuwa ni jambo jema sana lakini ikifungwa itakuwa ni shida kubwa.
Binafsi ninaiombea Simba ishinde ili:
1. Amani ndani ya Club
2. Kurejesha heshima iliyopotea miaka 3
3. Kuleta furaha kwa wana Simba kwani wamekuwa wanyonge sana kwa Yanga misimu mitatu.
NB.
Yanga ikifungwa wataumia lakini sio kwa kiwango kikubwa kama itakavyokuwa kwa Simba