Kwa Mtaji wa 2.5M nitatoboa kwenye biashara ya uwakala?

Kwa Mtaji wa 2.5M nitatoboa kwenye biashara ya uwakala?

Habari wakuu

Naombeni ushauri kwa wale ambao mna uzoefu na hii biashara

Nina mtaji wa 2.5M nilioukusanya kwa lengo la kufanya biashara ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa kwa mitandao ya simu

Je nitafanikiwa kwa mtaji huo?

Biashara hii ina changamoto zipi?

Nizingatie mambo gani?
Pesa haijawahi kutosha kwenye biashara ya uwakala lakini unaweza kufanya ata kwa laki tano mkuu, kila la heri, umakini ni muhimu sana.
 
Mtaji huo unatosha kama utakuwa ndo float na cash on hand ukitoa Kodi, kununua simu za uwakala na laini zake,

Kikubwa kuwa makini kwenye kutuma na kutoa hela kwa mteja,

Epuka matapeli wanaokupigia kuwa hela itaongezeka, epuka sana,

Kuwa ngangari nipe hela nikuhudumie,

Kingine issue za chuma ulete zipo,

Good luck and work hard
Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom