Kwa mtaji wa 3.5M inatosha kuanzia duka la spea za TV, Radio, simu na vifaa vingine vya umeme?

Kwa mtaji wa 3.5M inatosha kuanzia duka la spea za TV, Radio, simu na vifaa vingine vya umeme?

Heri kwenu sote wanajukwaa mlioalikwa kwenye uzi huu kama nilivyonena hapo juu.

mimi ni kijana nipo kuomba ushauri juu ya biashara ya kufungua duka la spear ya vitu vya kieletronics kama ambayo baadhi nmevitaja juu..pia ikumbukwe mimi ni fundi wa hivyo vitu.

Eneo nililopanga kufungua ni kahama au katoro pia kama kuna sehem nyingine yenye watu wengi ambayo haina mafundi nijuzeni.

pia kama unajua chimbo la spear hizo nambie.

Nakaribisha maoni na ushauri, vifaa vya ufundi vipo.
Mkuu, dunia inabadilika kwa kasi sana..
Vifaa hivi vya kielectronic siku hizi vinatengenezwa kwa mfumo wa kukunyima uwezo wa kutengeneza mwenyewe kama kikiharibika,
Sasa imefikia ikiharibika simu, tv na radio unatupa maana havitengenezeki, na ukijaribu kutengeneza ndio unaharibu kabisa na tunaona jinsi mafundi walivyokuwa na maisha magumu siku hizi ya kugombana na wateja wao kwa kushutumiwa kuharibu zaidi badala kutengeneza hivi vifaa....
 
Hitimisho na ushauri?
Mkuu, dunia inabadilika kwa kasi sana..
Vifaa hivi vya kielectronic siku hizi vinatengenezwa kwa mfumo wa kukunyima uwezo wa kutengeneza mwenyewe kama kikiharibika,
Sasa imefikia ikiharibika simu, tv na radio unatupa maana havitengenezeki, na ukijaribu kutengeneza ndio unaharibu kabisa na tunaona jinsi mafundi walivyokuwa na maisha magumu siku hizi ya kugombana na wateja wao kwa kushutumiwa kuharibu zaidi badala kutengeneza hivi vifaa....
 
Hitimisho na ushauri?

Kama unaenda China mwenyewe...inaweza kuwa inatosha
Lakini kanunue vitu kama accessories ya vifaa vya kielectronic kama macover ya simu, screen protector, headphones, chargers, adapters, speakers ndogo, na vinginevyo ambavyo unauuza tu sio kutafuta kesi na wananchi
 
Asante ila unajenga hofu moyoni mwangu
Kama unaenda China mwenyewe...inaweza kuwa inatosha
Lakini kanunue vitu kama accessories ya vifaa vya kielectronic kama macover ya simu, screen protector, headphones, chargers, adapters, speakers ndogo, na vinginevyo ambavyo unauuza tu sio kutafuta kesi na wananchi
 
Naweza kuchangia mtaji wa M2 nambie upo tiari Kutoa share?katoro ni pazuri zaidi kwa hii shunghuli napafahamu vzr.
 
Mkuu uko wrong,Ukubwa wa mtaji sio ukubwa wa biashara.Biashara ni strategy.Unaenda katika eneo ambalo unajua biashara yako unaweza mkakati na unaanza mdogomdogo.

Unaenda kwa muuzaji wa jumla kwanza ili upate gharama za kununua na upange bei ya kuuza.Kisha unaweka mkakati wako wa mauzo kisha unakuwa tu na sample dukani then mtua anaagiza mzigo unapiga simu kwa muuzaji wa JUMLA kucheck kama mzigo upo unafanya biashara.KUWEKO STOCK kubwa dukani sio ukuwa wa biashara.Dukani ni showroom tu kwamba una huduma au bidhaa fulani.
Siyo kweli, Biashara ni mtaji huwezi kuniambia 3.5 anaweza kufanya biashara itakayoonekana na kukamata soko kiivyo, kuujua ukubwa na umuhimu wa mtaji ingia kwanza kwenye Biashara ndiyo utajua biashara yako inahitaji fedha kiasi gani ili iweze kujiendesha.
 
Kwa huo mtaji wako vifaa vya umeme achana navyo kabisa, Maana hutapata wateja
(wateja wengi wa vifaa vya umeme hutaka mzigo wa pamoja na sio kuzunguka zunguka)

Spea za Simu labda uchukue zile za Simu ndogo za mil.1 na afu za Simu kubwa kama za mil. 2.
Hapa uwe na zile za sample tena zile common TU
(ukiwa na ujuz wa kutengeneza Simu zitakulipa zaidi)

mf:maiki, SPIKA, system charge, IC, power buttons, na touch&display za Simu bei Chee zinazotoka Sana.

Vifaa vya redio na tv Hapa tenga laki 5 ili
Uwe na vile basic Kama SPIKA ndg,diode, transistor, soda waya,maganda ya SPIKA, power za sabufa, n.k

Ila ili uuze vizur jitahidi Hapa upate fundi au wewe mwnyw uwe fundi [emoji4][emoji120]
 
Good mkuu
Vifaa vya ki electonics vipo vingi sana
Kuna Ic,transistors na vikolombwezo kibao
Ushauri wangu kwenye hizo ic chukua ambazo zina tumikia nyingi mtaani utauza!
Vifaa vitauzika sababu matatizo mengi yapo yanatokea
Uchukue vile vinavyoleta shida sana
Na hi utagundua sababu wengi watakuj kuulizia ulizia mala nyingi
Million 3 nn pesa nyingi kwa kuanzia
Keep it up!
Nkupe mfano tda2050 dar 700 tu
Iriywanauza hadi 2000/2500
Hiyo 7265 huwez kuigusa kizembe wakat dar wanauza rahisi sana
Hizi 5551 ni 100 ila iringa ni 500 moja!
 
Kwann nasema vifaa vya umeme huwezi,

Hapa Kuna vitu vitaipukuta iyo pesa yako yote na hutojua imeishaje na vyote Ni muhimu.

Mfano,
kwaSasa Bei za waya TU kwa jumla ziko Kama ifuatavyo
[emoji117]1.5mmtwin inacheza 130,000-145,000
Kwa KUANZIA unatakiwa uwe nazo hata 5

[emoji117]1.5mmSingle inacheza 40,000- 45,000
Kwa KUANZIA unatakiwa uwe nazo hata 3

[emoji117]2.5mmtwin inacheza 200,000-210,000
Kwa KUANZIA unatakiwa uwe nazo hata 3

[emoji117]2.5mmsingle inacheza 70,000- 80,000
Kwa KUANZIA unatakiwa uwe nazo hata 3

[emoji117] 4mmtwin inacheza 350,000- 370,000
Kwa kuanzia Unapaswa uwe nazo hata 2

[emoji117]6mmtwin inacheza 470,000 - 500,000
Kwa kuanzia Unapaswa uwe nayo moja

[emoji117]10mm inacheza kwenye 850,000- 950,000
Kwa kuanzia Unapaswa kua nayo hata moja.

Hapo bado ujaja kwny
- M/switch (unatakiwa uwe nazo za Bei rahisi na za Bei kubwa (tronic)
Mf: pc moja ya 4way m/switch tronic inacheza kwenye 68,000 Bei ya JUMLA. 6way= 80,000 bado 8way japo hii haitoki Sana.

Bado ujaja tena kwenye
[emoji117]breaker (single&three phase),
[emoji117]cut out (single&neutral),
[emoji117]E/rod (kawaida&pure) ,
[emoji117]Conduit
[emoji117]lamp Switches (kawaida&tronic)
[emoji117]Dp switch (tronic&kawaida)
[emoji117]Cooker socket (tronic&kawaida)
[emoji117]switch Socket(kawaida&tronic)
[emoji117]clips , (conduit clips&cable clips)
[emoji117]Metal box
[emoji117]Surface box
[emoji117]Junction box
[emoji117]Round box
[emoji117]Elbows&bendings
[emoji117]Tester
[emoji117]Tape
[emoji117]Connector
[emoji117]Holder
[emoji117]ceiling rose
[emoji117]Taa (wat 3,5,7,12,20,28,38,48) rangi na fasheni tofauti tofauti (za kawaida na vallight)
 
Back
Top Bottom