Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Vifaa vya simu kama unaijua....bora ufanye hiyo.
 
Naunga mkono hoja
Huwa nina amini sana kufanya biashara kama kampuni ,ni rahisi kuaminika na kufanya kazi na taasisi mbalimbali na hata serikali, kipndi hicho nilikua nasoma magazeti ya mwananchi kwa nyuma kuna tenda mbalimbali zinatangazwa , ukiwa chini ya kampuni na ukapata connection ya wakurugenzi wa mikoa na hata viongozi mbalimbali unapiga kazi cha msingi usiwe mchoyo tu .
 
Kwa idea hizi tatu/nne
Mimi ningekushauri ufanye accessories tu
Nafaka Muda utakubana
Hardware mkuu huu mtaji sjui kwa huko kigoma ila utanunua vitu vichache sana utabaki na stress achana nayo
Vifaaa vya umeme ni nzuri ila mtaji pia mdogo

Ila pia take your time tafuta mazingira unayooishi changamoto zake uzitatue
Mind you biashara bila usimamizi wako mzee ni hutojua mtaji umeenda wapi , wafanyakazi wako hawawezi kuonea huruma pesa yako
You have to be there for your business
 
Hiyo biashara, tena kwa mtumishi....ni ngumu aseee plus huo mtaji utaishia kununua vifaa tu
Ila siddo wanakopesha mashine ukiwa na mwanzo mdgo , tena hiyo 12 ni nyingi mno, kuna kipndi nilivyomaliza chuo nilikua nakapesa kadogo tu nikaenda siddo nikachukua machine ya kutotolesha kuku, na friza la dawa nikafungua kampuni ya kusambaza vifaranga vya saso , layers kienyeji na broiler ila mimi nilifanya kama kampuni , deni walilokua wananidai nilirudisha ndani ya miezi miwili tu nikachukua na machine nyingne.
 
Mkuu hapa umetupa akili sisi ambayo tulikua hatujui
Kwaio inshort ni mpaka uwe tayari umeanza ndio nawaweza kukukopesha?
 
Hardware mtaji inabidi uwe ngapi hiv ili afanye vema
 
Sawa nakuelewa, japo sio wa kwanza, Kuna walimu na watumishi wengi ambao bado ni wafanyakazi lakini pia wanabiashara zao zimesimama kwahiyo sitakua wa kwanza mkuu.
 
Sawa mkuu, nimepanga nimuweke mke afanye kusimamia, mimi kazini natoka saa 7 kwahiyo naona muda utakuepo.
 
Sawa nakuelewa, japo sio wa kwanza, Kuna walimu na watumishi wengi ambao bado ni wafanyakazi lakini pia wanabiashara zao zimesimama kwahiyo sitakua wa kwanza mkuu.
Fanya unachokiamini mzeee
Risk ni muhimu kwenye maisha
Hio ni ela Mingi
Hizi ni comments tu , uku dedicate utatusua tu
Kwa msingi ipe mudaa Hio biashara
 
Hapo ndo umeharibu mtaji uweke mke kweli??? Sijui akili za waalimu ziko je,
Sijajua wewe familia yako unaiendeshaje mkuu, nimezaliwa kwenye familia ya biashara mzee wangu ana duka kubwa la nguo anatoa biadhaa zake Kenya au Uganda, anaesimama dukani ni Mama mzee yeye anasafiri jumatatu anarudi alhamis/ijumaa, kwahiyo mtu ambae anashida kwenye biashara ni Mama, na wamefanikiwa kwa kiasi chao na kumiliki asset nyingi tu hapo Mwanza, lakini kwa kipindi chote hicho tulipokua wadogo Mama alikua hawezi kutoa hata shilling 100 bila kumtaarifu mzee, hata tulipokua tunahitaji matumizi ya shule tulikua tunampigia simu mzee sio Mama, kwahiyo Mama ni kama msimamizi/mhasibu tu, sio kwamba nampa biashara Mwanamke alafu Mimi naenda kustarehe, biashara ni ya kwangu Mimi yeye anakua msimamizi kwa muda mchache tu nikitoka.
 
Muheshimiwa kumbe njia unayoo
Kwanini usiingie kwenye nguo?
System unayokabisa apo
Au kuna changamoto ambazo umeamua kuachana nazo
Binafsi kama kwenye familia kuna system ni kheri upite nayo kuliko uanze moja
 
Wewe endelea kulinganisha wake wa miaka ya 60s 70s na hawa wa kwetu wa miaka 2000, mueke ndo utaona tofauti zao, acha maisha ya kuiga kwa baba, baba ako kaishi generation tofauti na wewe unaishi generation nyingine.......we kopa pesa uweke mkeo mualimu utarudi jf na mada nyingine tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…