Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Maalim Seif siyo Wanachama tena

Na Mwamba wa Kaskazini

Jamaa mmoja aliwahi kuniambia sikia tu kitu inaitwa utawala bora au imba sana kuhusu hiyo kitu lakini ukiwa wewe ndio unatakiwa kutekeleza hapo kwa wengi vumbi kubwa hutimka.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe na Mgombea wake huko Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad wamekosa sifa za kuendelea kuongoza na hata kuwa wagombea wa chama hicho.

Hii inakuja kufuatia Ibara ya 11(4) ya Katiba ya Chama hicho Toleo la 2015 kusisitiza wazi kuwa mtu atakoma kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo iwapo atatangaza kuunga mkono mgombea wa Chama kingine wakati chama hicho kimeweka mgombea.

Kwa kauli hii ya Katiba na kitendo cha sasa cha Zitto na Maalim Seif kutangaza hadharani kuwa wanamuunga mkono mgombea wa Chadema wa Urais, Tundu Lissu, wakati Chama hicho cha ACT bado kina mgombea wake wa Urais, Ndugu Bernard Membe.

Kwa Katiba hiyo Maalim Seif amekoma kuwa mwanachama wa ACT na hivyo anakosa sifa za kugombea Urais wa Zanzibar. Zitto pia anaanguka kuwa mwanachama wa Chadema na hivyo anapoteza nafasi zote za uongozi kwenye chama hicho.

Sasa swali ni Je, wataenzi misingi ya utawala bora kwa kuenzi Katiba yao inavyosema na kujiengua katika nafasi na kinyang'anyiro wanachoshiriki?
 
Umeambiwa swala la ushirikiano lilijadiliwa katika vikao vya chama na si kuwa mwanachama mmoja kajiamulia mwenyewe kumuunga mgombea wa chama kingine. Kwa hiyo hili swala lilikuwa maalum na kifungu hicho hakija kiukwa.
Mbona CCM na TLP walifanya kikao pamoja?
 
tusubiri hizo kanini zingine zitungwe.

Mwaka huu Magombe mtahangaika sana sana,tatizo hamchoki mna zikwa huku mnazungumza watu wa ajabu sana nyinyi.
Kuanzia tarehe 29 mwezi huu mtaungana na CUF kuunda upinzani au Lipumba hawafai au yule mama tanzania. CCM karibuni upinzani.
 
Hahaha ndo maan me sina imani na upinzani ni waongooo...sijapata kuona, wanajikanyaga wenyewe...
Mimi kura yangu itaenda kwa Magufuli wabunge na Madiwani wa CCM maana ndo naona wanamchango kwa Taifa letu la Tanzania,
 
Wamfukuze fasta..ccm walikua sahihi kumfukuza sasa ni zamu yao nao wamtoe nduki
 
Mbona uko kimya kwa jpm anayevunja katiba daily? Au JPM yeye malaika?
Mkuu, unaoushahidi usiotiliwa shaka!? Hata hivyo, hawa jamaa wanatakiwa kuonyesha mfano...hawawezi kuwa kutwa kuchwa wanapiga zumari la kuwa kuna watu wanavunja sheria na katiba lakini wao ndiyo wa kwanza kuvunja sheria na katiba za vyama vyao.

Au ruksa kuvunja katiba ya chama ila ya nchi inawekwa kando!? Kama jibu ndiyo kwao, basi sisi watumia jicho la ziada tunauliza 'kama umeshindwa kuaminika kutunza na kukilinda kidogo (katiba ya chama) utaweza kweli kutunza na kulinda kikubwa (katiba ya nchi)!?
 
Duh hatari sana

Back
Top Bottom