Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma

Basi ni hatari sheikh wangu manake rais anaweza kulala akaamka na kumtangaza rafiki yake kuwa jaji mtu ambaye hana utaalamu wa sheria huoni kwamba hiyo ni hatari? Tufuate miongozo jamani kuendesha nchi kwa akili zako tutakuja kujuta.haya

Hiyo ndiyo katiba inayokuongoza!! "Katiba inaweza kumfanya rais wa Tanzania dikteta" - hiyo kauli hukuwahi kuisikia? Busara za Kiongozi aliyeko madarakani ndo zinahitajika. Hali iko hivyo toka tupate uhuru!!
 
Mmeumia sana kwa Mtela kupewa nafasi ya UDAS. Nikuulize swali mleta mada. Kwani Mkuu wa Wilaya ni Mtumishi wa Umma ama siyo?
Mkuu,soma hoja uilewe ndiyo ujibu na siyo kukurupuka kujibu hoja ilhal haujaielewe.
 
Huwezi kumuelewa huyu kwa vile hajui hata alichoandika. Hasira zote ni kwa vile Mtela Mwampamba kapewa UDAS
Sidhani kama umemuelewa mleta Mada,mleta mada ana hoja ya msingi na amefanunua vizuri il tumuelewe,labda ni kusaidie kutofautisha,UDAS unaupata kama U-mtumishi na Ukuu wa Wilaya unateuliwa bila kujal ulikuwa Mtumishi ilimradi tu ulikuwa mfia Chama cha Mapinduzi,kwa hiyo mleta Mada anahoji inakuwaje? DAS ateuliwe.
 
Kuna hoja za msingi sana katika bandiko lako lakini ni bahati mbaya unapoanza kuegemea mara kukomoa ukawa ndipo hapo unapoanza kupoteza njia. Kumbe angeteuliwa yeyote ambaye unahisi hana madhara kwa ukawa wala usingesema kitu. La msingi hapa ni kuangalia kama teuzi hizi zinafuata sheria, miongozo na kanuni za utumishi wa umma. Vinginevyo mteuzi atateua anaoona yeye wanafaa.
 

Haya ni maelezo mazuri kwa kilichotokea....Nadhani wahusika watasikia ...teuzi hizi za ma-DAS hazina budi kutenguliwa...JPM asikilize kilio hiki...Waliopendekeza uteuzi huu wanamhujumu RAIS...this is a very serious matter....Patronage, clientelistic tendencies and spoil systems katika teuzi za ma-DAS zisiruhusiwe kamwe...Hayo yafanyike kwenye teuzi za ma-DC na ma_RC lakini siyo katika ngazi za ma-DAS na ma-RAS....HAPANA, HAPANA, HAPANA...msaidieni Rais msimwangushe makusudi....
 
We kijana tulia sasa ulitaka makada wa ccm waliopigania chama kuingia madarakani watoswe? Na bado ofisi zote za serikali mpaka hapo kwenye ofisi yako ya CAG Ma Auditors watakuwa makada wa CCM... We endelea kuzungurusha tu mikono
kaka naweza pata wapi kadi ya ccm
 
Ulipigiwa kelele sana , labda kama unajifanya punguani kama kawaida yako.
 
Hv ni nani hata hivyo anaweza kuthibitisha kuwa huyo mteule hakuwa mtumishi wa umma?Mtu aweza kuutumikia umma kwa namna nyingi.Unaweza kumwona n mvuvı, mkulima,mchuuzı,mzururuji n.k lakn akawa bado n mtumishi wa umma.
Bado hujaelewa maana ya mtumishi wa umma au mtumishi wa Serikali
 
Una maanisha huyu ni yule jamaa aliyeangushwa na Lameck Airo?
We kijana tulia sasa ulitaka makada wa ccm waliopigania chama kuingia madarakani watoswe? Na bado ofisi zote za serikali mpaka hapo kwenye ofisi yako ya CAG Ma Auditors watakuwa makada wa CCM... We endelea kuzungurusha tu mikono
 
Watu wa nchi hii hawaeleweki hata kidogo, wanachojua ni siasa za kijinga, nasema za kijinga kwasababu zipo siasa nzuri. Mfumo wetu wa ajira upo vibaya na ushawahi kupigiwa kelele na vijana wengi humu kwakuwa ulikuwa hauwapi nafasi nyeti za kulitumikia taifa lao, tatizo kubwa lilikuwa neno ''experience'' hivyo kutoa mwanya baadhi ya watu kuwa na vyeo vingi, ilikuwa marufuku kwa kijana graduate kushika nafasi nzuri hata kama ni kipanga vipi. Hebu tujiulize leo yule kijana aliyotoka Mzumbe UDSM etc akiwa na GPA ya 4.7 ya P.A na ameweza ku demonstrate leadership skills kuliko jitu lililokaa kazini miaka 20 likiendekeza upendeleo, rushwa na uvivu kazini nani anastahili kupewa nafasi? Vijana mnajirudisha nyuma wenyewe kwa kuunga mkono mliyokuwa mnayapigia kelele.
Tumeshudia Rais mstaafu akichekwa na kulaumiwa kwa teuzi zake za kuwajazia vyeo watu wachache na kuminya fursa kwa wengine kupata ajira. Neno promotion limekuwa kichaka kibaya sana cha kuweka watu wenye uwezo mdogo sana, nimeshuhudia miaka ya 2005 mpaka 2009 watu wenye elimu ya UPE wakipewa nafasi nyeti zinazohitaji elimu ya juu na kuwaacha vijana na mi degree yao mtaani wakihangaika.
Fanya utafiti mdogo sana, angalia maafisa elimu wa ngazi zote nchi nzima, ukipata nusu yao wanastahili kuitwa maafisa elimu nahama nchi, nina uhakika wengi wao ni elimu ya hapa na pale.
Tatizo la leo ni Msaliti kuteuliwa ila sio dhamira ya dhati kuelezea utaratibu.
 
Kwa uteuzi huu wa makada hakutakuwa na tofauti kati ya DC na DAS,wote mbiombio na matamko
 
Kwa namna wanavyobadili ovyo makatibu wakuu wa wizara Tanzania wala huku chini sishangai. Sisi tunaamini yeyote anaweza fanya chochote muhimu cheti sahihi kwa nafasi utakayo zawadia either hiyo shahada yako inakupa knowledge or not.

Hakuna maendeleo kesho wala leo ndio kwanza watu wanajifungulia kwenye makorido ya hospital raia wanasaidia huku manesi wanaangalia (wote ovyo kuanzia mawaziri mpaka mfanyakazi wa front line) sioni sababu ya kulaumu mmoja wakati serikari kwa upande mkubwa inaviongozi wa aina moja most of whom are unqualified.

Poor tanzania
 
Kweli kabisa.
 
Ofisi ya mtumishi mkuu wa nchi (Rais), ina CCMISHA Utumishi wa Umma. Naona anajifunza kutoka China (One party policy). Kwamba tusubiri kidogo hata afisa elimu wa wilaya atatoka CCMUNI. Nadhani kuna kosa mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…