Kwa mujibu wa Standing Orders, DAS ni mtumishi wa Umma


Unahitaji kufanya tafiti zaidi kuliko generalisation. Sio sahihi hata kama una GPA ya juu kiasi gani, kutoka straight from UDSM sijui Mzumbe University ukapata cheo cha UDAS. Hakuna anayepinga vijana kupewa nafasi ktk utumishi wa umma, lkn ktk fikra zako jaribu kufikiri wale vijana wenye elimu hizo za UDSM au Mzumbe waliokuwa kwenye nafasi za chini, yaani chini ya DAS ktk wilaya husika waliokuwa wako kwenye succession plan ktk eneo husika wanavunjwa moyo kiasi gani. Tambua serikali ya Tanzania ina vijana wengi wasomi kwenye kada za chini wanaotakiwa promotions katika hizi kwa kupanda ngazi moja baada ya nyingine by merit sio upendeleo. Hawa vijana wako wengi ndani ya serikali yetu, hii ndio argument.
 
P.K kutoka Rwanda
Anataka ampe mifumo yote ya TRA atusaidie kweli ana washauri wazuri kweli? Na yeye anafikiriaga kabla kusema? Kuna siku atasema jeshi wakajifunze Kigali!
 
Ukisoma vizur hoja yangu utaona umejibu nilichokizungumza, kwanza nimeanza kwa kukosoa utaratibu wetu mzima wa ajira na vilivyomo ndani yake ikiwa na pamoja na hizo promotions, pia nikatoa mfano huo ambao ndio ulijengea hoja yako....kwanza sikatai promotion kwa waliopo kwenye utumishi tayar kwa kuwa ignore na kulazimisha kuleta fresh from huko Mzumbe, UDSM etc, nilichojaribu kuangalia ni kitendo cha baadhi yao kupandishwa vyeo wakati wameboronga sana na hawana hatab hizo elimu za kushika hizo nyazifa. Nimetoa changamoto ya baadhi ya nafasi ya afisa elimu kama wanaozishikilia wengi wao wanazistahili? Kama eneo husika wapo vijana wenye uwezo mkubwa sioni kama yupo kichaa anaweza akawaacha na kuleta freshers hapo, na pia vijana niliozungumza sija base kwenye GPA tu bali nimezungumza na ubora wake(uaminifu, uchapakazi na ubunifu ).
Naamini kabisa hoja ya uzoefu kazini ilitumika vibaya sana na ndio iliyopelekea watendaji wengi kutokuwa wabunifu.
 
Mahead master na mahead boy na mamonita na mamonitresi anawateua lini?
 
Katika historia ya utawala katika nchi hii cheo cha DAS kimekuwa kikibadilika jina na hata namna ya kuwapata kuna wakati waliitwa DAO(District Administrative Officer) baadaye wakaitwa DO(District Officer) baadaye wakarudia jina la DAO na kufuatia sheria ya Tawala za Mikoa wakabadili jina na kuwa DAS cheo hiki ni cha utumishi wa umma si cha kisiasa NAMNA YA KUWAPATA
Mwanzoni walikuwa wanateuliwa na Wizara ya Utumishi miongoni mwa watumishi wa umma wazoefu wengi wao walitokana na Maafisa utumishi au maafisa tawala wachache sana walitoka kada nyingine,wakati wa kuanza cheo cha DAS walichukuliwa waliokuwa ma DAO na baadhi ya watumishi wengine wakafanya mitihani,waliofaulu waliteuliwa kuwa Ma DAS kuna kipindi Utumishi walikuwa wanatangaza nafasi za U DAS watu walikuwa wanaomba na kufanya usaili lakini baadae utaratibu huu uliachwa Manejimenti ya Utumishi wa Umma wakawa wanateua miongoni kwa watumishi wa serikali kuwa ma DAS sasa kwa uteuzi wa juzi ni kitu kigeni inabidi wale ambao hawakuwa watumishi wa umma waingizwe kwenye utumishi wa umma maana cheo cha DAS ni cha utumishi wa umma lakini ingekuwa vema serikali kupitia Manejimenti ya Utumishi wa Umma wangetangaza nafasi hizi watu wenye sifa wakaomba na kufanya usaili maana inaonekana kama inaajiri hao MaDAS ombao hawakuwa watumishi wa Umna
 
Nyenyere njoo upate elimu, hizi standing orders miye nilizisoma zamani sana na naona huu mtifuano wa aliye mwema zaidi ya malaika mkuu Gabriel
 
Natamani na mimi nijue kuandika maneno yenye rangi kama hayoo yenye wekundu
 
Stop being too negative. Wewe unawafahamu sana wateuliwa kuliko mamlaka zao za uteuzi? Wakati mwingine tuache kufikiri kwa mazoea, tubadilike!
Mtela Mwampamba alipangiwa ualimu serikalini akakataa na leo amekuwa mzalendo???
 
Safi sana mkuu, naona wewe unazungusha kiuno kwa ufundi kabisaaaa!! Piga na push-ups kabisa, tutakujengea mnara
 
Mkuu jitokeze nikupe furushi la vileo ukajivinjari jumapili hii
 
Ki tafsiri na sheria uko sawa. Hebu katika awamu hii nitajie DEDs wawili tuu ambao sio makada wa Ccm. Awamu hii iliwapa makada wengi uteuzi bila kujali sifa wala sheria. Huyu DAS wa Kisarawe alikuwa kada wa Ccm mitandaoni hakuwa mtumishi wa umma ndio maana hakuwa na maadili. Hata sasa hana mahali pa kuwekwa labda akakae pale Lumumba kufanya kazi za mitandaoni
 
Hebu tujaribu kuupitia huu uzi.Nafikiri hiki ndicho kipindi muafaka kuangalia yanayotendeka na kanuni na miongozo tuliyojiwekewa.Sipingani na Mamalaka lakini tunahitaji ufafanuzi.
 
Hebu tujaribu kuupitia huu uzi.Nafikiri hiki ndicho kipindi muafaka kuangalia yanayotendeka na kanuni na miongozo tuliyojiwekewa.Sipingani na Mamalaka lakini tunahitaji ufafanuzi.
Mkuu kila kitu ndani ya uzi huu kabambe kimerekodiwa kwa ajili ya ushahidi
 
With all the skill set I like this one 'stress management skills '
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…