#COVID19 Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Tunapoteza watu kwa kiwango kikubwa kutokana na Corona

#COVID19 Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Tunapoteza watu kwa kiwango kikubwa kutokana na Corona

Ukitaka kujua kuwa hasingiziwi zingatia:

1. Tofauti ya takwimu za vifo 2019 na 2020.
2. Tambua jitihada za serikali kuficha takwimu za Corona Apr 2020.
3. Zingatia idadi ya misiba uliyoisikia wewe kuhusiana na Corona ndani ya mwezi mmoja.
4. Jiulize "nane nane" inafanyika lini?
5. Mbio za mwenge zimefika wapi?
6. Kumbuka tuko ushetu kwa mazishi bila kusahau:

View attachment 1885941

Ukimaliza tafuta wa kwako wa kusingizia.
Mkuu, kama ni hivi basi ni kutishana. Kwa hilo moja tu la Mwenge, inatosha kusema vitisho sasa ndo vinavyotumika!

Waulize Bahi na Chamwino wameupokea mwenge lini? Wiki iliyopita tu wala si mbali.
 
Kwa mawazo yako haya ni mapambio:

Ni upumbavu uliopitiliza kudhani kuwa watu hawafi kwa sababu tu wewe hujafiwa.
Ni upumbavu pia kudhania kila nayekufa ni korona
 
Wewe kama siyo kipofu, utakuwa mnafiki; kama mnafiki, utakuwa na ulemavu wa akili. Ni wapi ambako misiba haijaongezeka zaidi ya ilivyozoeleka?

Kesho, huku anazikwa Waziri wa ulinzi, jioni hii kuna misiba mingine mitatu. Wewe unaona hii ni kawaida. Na mwenyeji hapa anasema kuwa leo ni afadhali maana siku hizi, karibia kila siku ni 6 kwenda juu.
Achaa uwoga wwe, kila siku lazima watu wafe,na kila siku lazima kuna watu wanazaliwa!!
 
Takwimu za kupika ambazo hazi relate na mtaani!!!!

Tunapita makaburini hatuoni hao watu wakizikwa.Kama mmekula hela za watu rudisheni.

Hao ndugu zenu mnajua kabisa wengine wana ma Tb,cancer lakini wakifa mnataka kusema Corona ndo primary source.

Haya pikeni pikeni data zenu huko,wazungu wafurahi mkiona watu hawalewi somo pandeni ndege mkaulize nchi jirani wanawezaje kupika data na kuwatia uoga wananchi wakati huo huo wanakula hela za waZungu kiulaini

Mfuateni mseveni awafundishe kuzika matambala/migomba ili mle hela za wazungu vizuri msisumbue wananchi.
Haya majibu ya kipuuzi kabisa. Kwamba kwakuwa wewe hujafiwa na mtu, basi hakuna Corona.
 
Mkuu, kama ni hivi basi ni kutishana. Kwa hilo moja tu la Mwenge, inatosha kusema vitisho sasa ndo vinavyotumika!

Waulize Bahi na Chamwino wameupokea mwenge lini? Wiki iliyopita tu wala si mbali.

Wanaotishwa watoto wadogo tena wasiopenda kunywa uji?

Kutishwa maana yake nini? Mbona kujidhalilisha hivyo?
 
Ni upumbavu pia kudhania kila nayekufa ni korona

Ni upumbavu uliopitiliza wa kiwango hiki:

IMG_20210718_063455_991.jpg

kudhani kuwa tofauti ya vifo baina ya 2019 na 2020 haikuletwa na Corona.

NB: Kwenye bold pana kuhusu sana.
 
Hakuna anayepinga kuwa covid-19 ipo, chanjo imeletwa na mpaka sasa ni hiari. Ili wote tuongee lugha moja, mamlaka hazina budi kuja na muongozo unaoeleweka hadi kwa wenzangu wa Nanjilinji kule ambao hawakuwahi kuijua shule.

1. TZ yote, ina jumla ya vifo vingapi kwa siku?
2. Kabla ya corona, vifi vilikuwa vingapi kwa siku?
3. Kabla ya corona, ni magonjwa yapi yaliongoza kuua?
4. Corona imeongeza vifo vingapi kutokea kwenye wastani wa kabla yake?
5. Tunajua chochote kuhusu vifo vingapi vimesababishwa na corona tu na vile ambavyo corona imemalizia kazi ya magonjwa mengine?
6. Hakuna wanafunzi wanaokufa kwa corona?
7. Tuelimishwe, kwanini corona haiwashambulii watoto wadogo?
9. Corona inauwa wale walio na access na mitandao tu?
10. Maeneo gani ya nchi yameathirika zaidi na corona? Sisikii taarifa za kutoka mikoa kama ya Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Mara, Lindi, Mbeya, Rukwa, n.k Ni Dar na watu mashuhuri mashuhuri tu.

Mtaani kwetu, vimetokea vifo vitatu kwa tangu corona iingie, vyote ni mwaka huu, vyote ni wanaume walio juu ya umri wa miaka 40, wote walikuwa wagonjwa kabla, Moyo, Figo na Sukari.
 
Kwahiyo wewe kwa akili yako ulikuwa unawaza ya kwamba huyo mzee ataishi everlasting life ama ?

Na hiyo corona yako inaua wengine tu wewe haikuui ?

Ilikuwa Dar siyo Tanzania. Sasa uko kwenye kuhalalisha watu kufa. Full kuruka ruka kama bisi.

Hata mumiani hufanya hivyo hivyo.

Sababu za kufa ziko wazi:

IMG_20210809_101955_435.jpg

Wewe ni sehemu ya hawa mnaopaswa kuwajibishwa kwa vifo hivi?
 
Takwimu za kupika ambazo hazi relate na mtaani!!!!

Tunapita makaburini hatuoni hao watu wakizikwa.Kama mmekula hela za watu rudisheni.

Hao ndugu zenu mnajua kabisa wengine wana ma Tb,cancer lakini wakifa mnataka kusema Corona ndo primary source.

Haya pikeni pikeni data zenu huko,wazungu wafurahi mkiona watu hawalewi somo pandeni ndege mkaulize nchi jirani wanawezaje kupika data na kuwatia uoga wananchi wakati huo huo wanakula hela za waZungu kiulaini

Mfuateni mseveni awafundishe kuzika matambala/migomba ili mle hela za wazungu vizuri msisumbue wananchi.
Una very low IQ
 
Ni upumbavu uliopitiliza wa kiwango hiki:

View attachment 1885976

kudhani kuwa tofauti ya vifo baina ya 2019 na 2020 haikuletwa na Corona.

NB: Kwenye bold pana kuhusu sana.
Kufa kwanza wewe ndo tujue korona inaukubwa gani ,maana mnakomaaa kama vile watu walikuwa hawafi hapo nyuma ,korona ipo lakini mnajaribu kuikuza mpaka watu waogope kwenda kufanya shughuli zao.mbona nyinyi hamfi kila siku tunawaona jf .
 
Nmekuja hapa chuoni kuchkua cheti na nmekua hapa kwa wiki moja, nmeshuhudia vifo vya maprofesa watatu ndani ya wiki moja, na mmoja kafariki leo asubui. Anasema data za kupika asubir siku wakidondoka ndugu zake ndo ataamini. Ofkoz hali sio nzuri.
Watu wanatamani kukimbia mikataba yao waache kufnya kaz za kuhudumia public,
Hapo hapo chuoni ndo pa kuanzia na takwimu za vifo vya corona.

Vipi wanachuo wao hawafi kwa corona ni maprofesa tu ?

Mie nitaungana na njia alizotumia Magu kupambana hili dude la kupikwa.
Kwa nchi hii hali ingekuwa mbaya zaidi kwenye mashule yetu na vyuo, lakini hakuna vifo.
 
Jana Mh. Zitto Kabwe akiongea na wanahabari, aliweka wazi takwimu za vifo vinavyosababishwa na Covid 19 kwa sasa nchini mwetu, na kwamba kwa sasa ni vifo 509 kwa wiki, ikimaanisha ni wastani wa vifo 73 kwa siku.

Takwimu hizi zinafahamika kwa watawala, maana chanzo chake ni kwenye mamlaka za Serikali, ikiwemo Wizara ya Afya, lakini wote wamepatwa na kigugumizi kuziweka wazi kwa kuhofia aibu watakayoipata baada ya muda mrefu kutangaza kuwa Covid 19 haipo Tanzania au ipo kidogo sana. Lakini wasichojua ni kuwa mficha maradhi, kilio humwumbua.

Ifahamike kuwa hivi ni vifo vilivyothibitika kwenye hospitali, bado wale wanaofia majumbani na kwenye zahanati. Na hili halishangazi, linaonekana wazi kutokana ja kuwepo taarifa za misiba kila mahali, na kila siku.

Kwa wastani wa vifo 73 kwa siku, Tanzania itakuwa ndiyo inayoongoza kwa vifo vya Covid 19 barani Afrika, na ya tatu Duniani baada ya Mexico (vifo 172) na Thailand yenye (vifo 149) kwa mujibu wa takwimu za leo.

Yaani wakati Dunia ikishuhudia kupungua kwa kiwango kikubwa cha vifo vinavyosababishwa na Covid 19, Tanzania inapaa kwa mwendo wa ajabu kwa vifo vya Covid 19. Haitachukua muda, kwa namna tunavyoenda, Tanzania itaongoza kwa vifo vya Covid 19 Duniani.

Kila mwenye akili achukue tahadhari, mjinga ataangamia na ataangamiza wengine kwa ujinga wake.

Tunawomba Mungu akaweke baraka katika jitihada tunazozifanya kwa dhamira.
 
Hivo ni vifo vinavyo sajiliwa serikalini, je wakijumlisha na vifo vya vijijini visivyo sajiliwa. Takwimu ya vifo inaweza ikafika hata 300 kwa siku moja.
 
Ni ugonjwa wa COVID 19 pekee duniani uliowahi kutangaza vifo vya watu kila siku. Malaria, kansa, shinikizo la damu, vifo wakati wa kujifungua n.k havijawahi kutangazwa ingawa tulikuwa tukizika wapendwa wetu kama kawaida
Hivi ni kweli kwamba China watu hawafi tena?

Za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Hakuna anayepinga kuwa covid-19 ipo, chanjo imeletwa na mpaka sasa ni hiari. Ili wote tuongee lugha moja, mamlaka hazina budi kuja na muongozo unaoeleweka hadi kwa wenzangu wa Nanjilinji kule ambao hawakuwahi kuijua shule.

1. TZ yote, ina jumla ya vifo vingapi kwa siku?
2. Kabla ya corona, vifi vilikuwa vingapi kwa siku?
3. Kabla ya corona, ni magonjwa yapi yaliongoza kuua?
4. Corona imeongeza vifo vingapi kutokea kwenye wastani wa kabla yake?
5. Tunajua chochote kuhusu vifo vingapi vimesababishwa na corona tu na vile ambavyo corona imemalizia kazi ya magonjwa mengine?
6. Hakuna wanafunzi wanaokufa kwa corona?
7. Tuelimishwe, kwanini corona haiwashambulii watoto wadogo?
9. Corona inauwa wale walio na access na mitandao tu?
10. Maeneo gani ya nchi yameathirika zaidi na corona? Sisikii taarifa za kutoka mikoa kama ya Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Mara, Lindi, Mbeya, Rukwa, n.k Ni Dar na watu mashuhuri mashuhuri tu.

Mtaani kwetu, vimetokea vifo vitatu kwa tangu corona iingie, vyote ni mwaka huu, vyote ni wanaume walio juu ya umri wa miaka 40, wote walikuwa wagonjwa kabla, Moyo, Figo na Sukari.

Unaandika tu au pia wajiuliza waandika kutokea wapi?

IMG_20210808_154317_100.jpg

(a) Unaisoma na kukuelea vilivyo?

Nikushauri uisome tena ikuelee halafu uangalie ulichoandika kiasi gani ni utopolo. Labda tuanzie hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom