Hakuna anayepinga kuwa covid-19 ipo, chanjo imeletwa na mpaka sasa ni hiari. Ili wote tuongee lugha moja, mamlaka hazina budi kuja na muongozo unaoeleweka hadi kwa wenzangu wa Nanjilinji kule ambao hawakuwahi kuijua shule.
1. TZ yote, ina jumla ya vifo vingapi kwa siku?
2. Kabla ya corona, vifi vilikuwa vingapi kwa siku?
3. Kabla ya corona, ni magonjwa yapi yaliongoza kuua?
4. Corona imeongeza vifo vingapi kutokea kwenye wastani wa kabla yake?
5. Tunajua chochote kuhusu vifo vingapi vimesababishwa na corona tu na vile ambavyo corona imemalizia kazi ya magonjwa mengine?
6. Hakuna wanafunzi wanaokufa kwa corona?
7. Tuelimishwe, kwanini corona haiwashambulii watoto wadogo?
9. Corona inauwa wale walio na access na mitandao tu?
10. Maeneo gani ya nchi yameathirika zaidi na corona? Sisikii taarifa za kutoka mikoa kama ya Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Mara, Lindi, Mbeya, Rukwa, n.k Ni Dar na watu mashuhuri mashuhuri tu.
Mtaani kwetu, vimetokea vifo vitatu kwa tangu corona iingie, vyote ni mwaka huu, vyote ni wanaume walio juu ya umri wa miaka 40, wote walikuwa wagonjwa kabla, Moyo, Figo na Sukari.