Kwa Muktadha na kwa uchambuzi wa kina CCM ndio taasisi pekee itakayolinda maslahi mapana ya JMT

Kwa Muktadha na kwa uchambuzi wa kina CCM ndio taasisi pekee itakayolinda maslahi mapana ya JMT

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Nikiwa kama mkongwe katika siasa za chini kwa chini au ndani kwa ndani leo tena narudi kwenu watanzania wazalendo kuwakumbusha kuwa kamwe hakuna Chama chochote cha Siasa ambacho kitaleta mabadiliko ya kweli na ya enzi zaidi ya C.C.M. kwa maslahi ya wanyonge.

Nilipokuwa kijana sana nilianza na mihemuko ya kuichukia CCM lakini kwa muda mfupi sana nilikuja kutambua kuwa CCM ndio taasisi imara na iliyojengwa mahsusi kwa ukombozi wa Taifa .

Sikatai kuwa zipo nyakati CCM inaingiliwa na mabaradhuli ,wahuni,wakwasi,walami na marahamia ili kutaka kuiteteresha na kuimaliza ....hii ni kawaida kwa taasisi kubwa ....
Lakini mfumo wa CCM unaiwezesha kuwatemesha bungo wote ambao ni ghasia kwa jamii.
Mwalimu Nyerere alipewa mrejesho na wananchi ya kuwa hatuhitaji mfumo wa vyama vingi lakini kwa busara zake na pengine analysis aliyopelekewa nyakati hizo aliona si busara kuendelea na makabiliano makali na walami na hivyo akaamua kupindua matokeo na kusema tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi.....

Msimamo wangu hadi mwisho...tunatakiwa kurudi kwenye utawala wa chama kimoja kama china hivi.

Kwa uchambuzi wangu toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi sijaona ladha au idea mpya yoyote iliyowahi kuletwa mbele ya meza ya wananchi ili wachague kati ya yale yaliyoahidiwa na TANU/ASP au CCM ...versus ideas mpya ya vyama vingi.
Kwa ufupi ni kwamba yote yaliyokuwa yanashughulikiwa na mfumo wa chama kimoja ndio hayo hayo yamekuwa ni mahitaji katika era ya vyama vingi ...hakuna jipya linaloombwa au kulalamikiwa.

Kwa muktadha huu na kwa kutumia sayansi na mantiki sijaona jipya lolote ambalo limeletwa na vyama vingi katika kuboresha maslahi ya wananchi wanyonge .
Hitimisho langu kitakwimu na kimantiki ni kwamba tunaweza kuendelea kudai ,kuboresha na kushuhudia mambo mazuri tukiwa na mfumo wa chama kimoja ...tena bila kuuana na kuletewa taharuki kupitia wanaharakati wanaolipwa kuvuruga nchi...
Leo naishia hapa....

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!

Hongera GODBLESS LEMA
RiP ALUTE
 
Back
Top Bottom