Kwa muujibu wa sheria ya habari ya mwaka 2016 kifungu cha (19)1 kinaeleza waajiriwa wa vyombo vya habari kusoma na sio mtu wakawaida haruhusiwi kutoa

Kwa muujibu wa sheria ya habari ya mwaka 2016 kifungu cha (19)1 kinaeleza waajiriwa wa vyombo vya habari kusoma na sio mtu wakawaida haruhusiwi kutoa

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
20250206_130457.jpg


Nimesikia kauli iliyotolewa bungeni na waziri naibu wa habari, tamaduni na sanaa na michezo Hamis mwinjuma kwamba wachambuzi wote lazima waende shule kwanza ambapo amedai kwamba ni kutokana na sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kifungu cha (19)1,

Katika uhalisia sheria haikumaanisha wachambuzi wote ila wale wahudumu wa vyombo hivyo yani waajiriwa na sio kila mtu kutoa uchambuzi kwenye vyombo hivyo kuhusu suala flani harusiwi huku kuna minya uhuru wa kujielezea nazani waziri anapaswa kupitia sheria upya na kuelewa kilicho andikwa.

Kwa muujibu wa kifungu cha sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kifungu cha (19)1 kinawataka wahudumu yani waajiriwa wa vyombo vya habari kusoma kozi fupi kwanza kabla ya kuajiriwa lakini hakimaanishi kwamba mtu wa kawaida hawezi kutoa habari kwenye vyombo hivyo.

Nukuu ya Naibu waziri mwinjuma bungeni " wachambuzi hawapendi kulisikia jambo hili, lakini ni ukweli usiopingika kwamba hili linapaswa kufanywa kwasababu lipo kwa muujibu wa sheria inataja kabisa watu wanaopaswa "kukaa kwenye vyombo vya habari" na vigezo wanavyotakiwa kuwa navyo kabla ya kuruhusiwa kufanya hivyo"

Naomba ieleweke kwamba kukaa kwenye vyombo vya habari na kutoa habari sio kosa kisheria kwa mujibu wa sheria za vyombo vya habari ila sheria hiyo inataka waajiriwa kusoma na sio mtu wa kawaida haruhusiwi, kwasababu huku kunaweza kuminya uhuru wa kijielezea na haki za binadamu, huku nikutafsiri sheria vibaya pasipo kufikiri.
 
Back
Top Bottom