Kwa mwamko huu, CCM hawawezi kukubali Katiba Mpya

Kwa mwamko huu, CCM hawawezi kukubali Katiba Mpya

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Amini nawaambia kabisa kuwa CCM siyo wajinga kiasi hicho.

Kama watawala wanafuatilia mikutano ya CHADEMA kuhusu katiba mpya naamini wanalo jambo moyoni mwao.

Siamini kama watakuwa tayari kukubali kupitisha katiba mpya ya kweli kwa nia safi kabisa.

Mikutano yote ya CHADEMA imekuwa na mutikio chanya wa wananchi wasomi na kina maamuuma.

Inaonyesha sasa watanzania wameanza kuelewa maana ya upinzani na wapo tayari kuitupilia mbali CCM.

Hapa ni Mpanda ambako CCM huwa inajivunia kupata wapiga kura wengi kila uchaguzi.


 
Uko sahihi sana kamanda...mpanda imeitika aisee

IMG-20230523-WA0118.jpg
 
Boss kaomba mapema kuwe na mipaka miwili🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nje ya hapo anaweza kuona maingasungura 2025
 
Haya mambo ya katiba mpya sidhani kama yna afya kwa sababu mwisho wa siku tutajikuta tuna tatizo la aidha serikali moja au tatu. Mimi nashauri kwamba katiba mpya iandikwe ya Tanganyika nchi peke yake alafu Zanzibar nao waandike yao kisha tuulizane tunataka muungano a aina gani? Nchi moja pia ni hatari sana ni bora tufanye muungano wa federation au kama huu wa jumuiya ya Afrika mashariki tu. Hapa kila nchi itakuwa na furaha tuachane na huu ulaghai wa 1+1= 3
 
Tunataka Fedha za Miradi kutoka IMF…hizi picha ni muhimu sana kwa Comrade Mwigulu Nchemba kwny kukamilisha project paper


'Demokrasia imeimarishwa sana katika kipindi hiki ikiwemo kuruhusu mikutano ya Siasa ( angalia kimbatisho)'

Tunawashukuru sana wana maridhiano wenzetu wa upande wa pili kwa kazi hii
 
Back
Top Bottom