Mngelijua zamani mama zetu walikua wanaambiwa utaenda kwa Fulani uwe unataka au hutaki, msingekua na haja ya kubisha. Baba zetu nao walikua wakitoka jandoni tu anapewa eneo la kulima nakukabidhiwa mke. Walikua wanakutana wakati mwingine kitu ambacho mwanamke alikikuta ndani ni jamvi la kulalia na majembe, na maisha yalisonga.
Japo kulikua na talaka lakini ni kwakiwango cha chini sana. Dada zanguni kama mlivyosema vigezo ni muhimu sikatai, ila kigezo cha kusema mwanaume lazima awe na kipato siafiki.
NYUMA YA KILA MWANAUME MWENYE MAFANIKIO KUNA MWANAMKE MWENYE HEKIMA
Utajivunia kipi kwa mumeo kudhihirisha wewe ni mwanamke unayejitambua? Anza nae maisha akiwa hana kitu (japo wapo wanaume waliojijenga kwanza) ili atamani kuendelea kukuona.
Ukimkuta tayari ana kitu halafu ukakosea mahali na uchumi ukayumba atakuona huna tofauti na mwanamke (kumbuka kwenye ndoa hakuna mwanamke, ni mke) HATA WANAUME TUNATAMANI SANA KUWA NA MKE MWENYE PESA LAKINI TUNATAKA TUJUE, UCHUMI UKIYUMBA MTATUSAIDIA NJIA ZA KUPAMBANA AU NDIO NYODO ZITAANZA.
By the way, hiyo zamani sikuwepo ila niliona aina ya maisha waliyoishi wanandoa enzi za utoto wangu.