Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kusudio la kuanzishwa, kufunguliwa na kuhuishwa kwa shirika mama la usafiri wa anga la nchi yetu pendwa
Tanzania ilikuwa lijiendeshe kibiashara, lipate faida na liweze kujisimamia na kujihudumia lenyewe bila kuwa mzigo kwa serikali.
Shirika la ATCL limekuwa na flight cancellation za mara kwa mara zisizo na kichwa wala miguu, yote hayo ni sababu ndege ziko busy kufanya Safari zisizo za kibiashara.
Leo utasikia kuna uhaba wa ndege, ndege zote zimeenda service, lakini ukifiatilia itakuwa ziko kwenye ziara za kuwazungusha walao neema za nchi na kuku ya Taifa wao na familia zao.
Hakuwa na sababu na IGP kutumia ndege ya biashara kwa Safari zake za kikazi, angetumia helikopta ya polisi ingekuwa vyema zaidi.
ATCL ikiendelea na utaratibu huu wa kuwa chombo Cha starehe kwa watu fulanifulani, itarudi kaburini mapema mno.
Kuwa na fleet nyingi sio mafanikio, mafanikio ni kuwa na fleet zenye kuwahudumia watu wengi zaidi ndio maana ndege za PW zinajaza wakati ATCL ndege zao zinaenda mswaki.
PW hawategemei ruzuku, wapo angani kila siku, wanafanya biashara seriously, huwezi walinganisha na ATCL.
MSIPOBADILIKA, NECHA ITAWAONDOENI SOKONI