mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 340
- 359
Wakuu habarini za kitambo kidogo na poleni sana kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na mpendwa wetu Rais Mstaafu Mzee Benjamini Mkapa (R.I.P),
Kwa muda mrefu huko nyuma nilikuwa najiuliza inawezekanaje na ni kwanini CCM hujikuta wanatumia nguvu kubwa sana kuvuka na hatimaye kupata ushindi wa chaguzi mbalimbali,
nimekuwa nikijiuluza pia ni kwa namna gani chama imara kama hiki, kikubwa na chenye historia ndefu kinawezaje kusumbuliwa na vyama vidogo na wakati mwengine vyama vipya kabisa kama vilivyoibuka kama CHADEMA, ACT WAZALENDO na vinginevyo
NILICHOJIFUNZA
CCM ni ama imelewa nguvu za madaraka au haihitaji kuendana na wakati nhususani mahitaji husika ya wananchi katika chaguzi zao za ndani wanapotaka kuchagua mwakilishi wao kwenda kushindana na wa vyama vingine.
chaguzi za ndani ya chama hiki kikubwa maarufu kama KURA ZA MAONI ni kichocheo kikuwa sana cha CCM kujikuta wanatumia nguvu kubwa kuwanadi wagombea wao katika chaguzi za kiserikali
nimejifunza kuwa chaguzi za kura za maoni CCM ni kielelezo namba moja cha chama hicho kujichimnbia kaburi la kupata washindani wabovu kulinganisha na vyama vingine, hii inatokana na ukweli wa namna michakato ya chaguzi hizo inavyopatikana ikwemo upigwaji wa kura, muda wa kujinadi, ufahamu wa wajumbe kuhusu wagombea, matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo na mzizi mkuu RUSHWA
nimefuatilia chaguzi nyingi zilizopita namna wajumbe walivyowanyoa wagombea ambao walipewa chinin ya dakika 3 kujinadi ambapo kundi kubwa la wagombea hao waliambulia kura 0 na wengine namba za viatu
MTIHANI WA RUSHWA
sijui kama TAKUKURU wanaweza kunikosoa kwenye hili, lakini kwa dhahiri shairi na kwa macho tu ya kawaida, haikuwa rahisi kwa mgomea wa CCM akashinda kura za maoni kama hajatoa kiasi kikubwa cha pesa kulinganisha na wagombea wenzake.
tafiti zisizo rasmi zimeonyesha pasi na shaka namna Wabunge wanaotetea nafasi zao, wafanyaiashara wakubwa, na watu wengine wenye uchumi mkubwa walivyoweza kushinda kura za maoni bbila kujali uwezo wao wa kuchambua masuala yanayowahusu watu wanaotaka kuwawakilisha.
hii ndio kusema kwamba linapokuja swala la kura za maoni, wajumbe wa kura hizo wa CCM hufumba macho yao kuchagua kiongozi mwenye uwezo na badala yake huangalia nani amewapa nini kumzidi nani...HATARI SANA HII
MAJUNGU NA FITNA
katika somo kubwa lingine ni uwezo wa wagombea wengi walioshinda na kushindwa kura za maoni kutengeneza uwongo na majungu dhidi ya wagombea wenzao wanaohisi kuwazidi vigezo vya ushindi ama uteuzi katika vikao vya juu.
udhaifu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ngazi za wilaya na mikoa umewafanya wagombea walioshinda ama kushindwa kufanikiwa kuwatengenezea tuhuma wenzao wanaohisi kuwa wanaweza kuwazidi sifa za kuteuliwa hivyo kuwatengenezea wakati mgumu.
MJADALA UMEFUNGULIWA