Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
halafu ndo yule msemaji wetu mwenye utapia mlo utamkuta anawasihi mashabiki kwenda uwanjani kuishabikia team yao, kwa mpira gani sasa? Mechi zimeshachezwa mezani tuje uwanjani kufanya niniTufikie hatua tuwe wakweli tu. Hii michezo tunayofanya haijengi team na wala hatujui ubora halisi wa kocha.
Tuambiane tu ukweli. Kwenda kucheza na teams ambazo tayari tumeshazinyong'onyesha kunatuondolea utimamu wa miili na akili tukija pambana na teams za ukweli.
Tumefikia hatua sisi wengine hata tukifunga bao 6 tunaona ni jambo la kawaida kwa teams ambazo tunacheza nazo sababu zinakuja tayari zikiwa zimeshashindwa toka nje haziji kushindana. Hivyo kocha anakosa muda wa kupanga mbinu za ukweli. Sababu hatuna ushindani kwa teams nyingi tunazocheza nazo ukiacha mikia na azam ambao tulivurugana nao.
Haya mambo hayatusaidii, hayaisadii team. Yanailemaza na kuidekeza. Tuacheni kupanga matokeo tena wazi wazi kabisa. Hata mtoto mdogo anaona. Mkisema mimi siyo yanga sijali sababu hata mkisema ni yanga haibadilishi chochote. Ila ukweli nitasema. Niueni nimekaa pale.👉
Simama uoneNiueni nimekaa pale.👉