Kwa nchi yenye matatizo makubwa ya maji, tunaruhusu vipi swimming pools?

Nadhani tutawaonea wenye swimming pool kwanini hatuvuni maji katika reserve dams yote yanapotelea baharini wakati na hii global warming bahari inapata maji toka North Pole milima ya barafu inayeyuka.

Tuna bahati na kuwa na maziwa makubwa sana duniani Tanganyika Victoria Nyasa kwanini hatuchukui maji uko kwenye vyanzo vikubwa sana vya maji tubabaki kulilia tu mvua ikichelewa kidogo sana.
 
Ni ya kufundishia watoto kuogelea ni kama viwanja vya futiboli vikapu nk. Ndio tutakapoibua waogeleaji wa kwendacolompiki.
 
Sisi wa kanda ya ziwa hatuwezi kuhangaika kuogelea kwenye vidimbwi vyenu mnaviita swimming pool, hivyo ni spesho kwa watu wa Dar ambao hawawezi hata kutembea kwenda kuogelea baharini....
 
Tanzania hatuna tatizo la maji, bali akili zetu ndio maji.
 
Tanganyika haijawahi na haitotokea kuwa na matatizo ya maji. Kilichopo ni Selikari mfu ya CCM ndio imeshindwa kufikisha maji kwa wananchi ieleweke imeshindwa kufikisha sio kuwa hayapo, nchi hii ina hadhina ya maji kuliko nchi yoyote duniani.
 
Ulishawahi kusikia Misra kuna uhaba wa maji wala umeme?
Hawana kabisa uhaba huo na wako jangwani na tena hupangia source ya maji hayo matumizi eti wasijenge mabwawa ka Ethiopia na hata Tanzania wanakubali tu
 
Mipango mibaya ya serikali ya ccm,nini kinazuia mji wa singida kujenga mabwawa ya kuvuna maji ya mvua?jiji kubwa la cape town linategemea mabwawa ya maji yatakanayo na mvua!jiji kubwa la joberg maji mengi yanatoka pale vaal dam!tuendelee kusubiri meli yetu ya Noah pale KIA.
Kuliko wachukua 5bn kujenga bwawa linaliweza kuhudmia Thousands of Citzen bora watumie hizo pesa kununua mpinzani, kumuwinda Diwani wa chadema na kurudia uchaguzi wa Bn 10.

Hii nchi kama haijalaaniwa basi inaongozwa na viongozi wenye laana
umehitimisha vema Mkuu
 
Sisi wa kanda ya ziwa hatuwezi kuhangaika kuogelea kwenye vidimbwi vyenu mnaviita swimming pool, hivyo ni spesho kwa watu wa Dar ambao hawawezi hata kutembea kwenda kuogelea baharini....
Ziwa mko nalo karibu

Mna shida ya maji

Wakinamama wanabeba ndoo za maji mpk

Vibiongo vimewatokeza

Ova
 
Hawana kabisa uhaba huo na wako jangwani na tena hupangia source ya maji hayo matumizi eti wasijenge mabwawa ka Ethiopia na hata Tanzania wanakubali tu
Yale ni mataifa yaliobarikiwa
 
Tanganyika haijawahi na haitotokea kuwa na matatizo ya maji. Kilichopo ni Selikari mfu ya CCM ndio imeshindwa kufikisha maji kwa wananchi ieleweke imeshindwa kufikisha sio kuwa hayapo, nchi hii ina hadhina ya maji kuliko nchi yoyote duniani.
kweli maji yamejaa tele
 
Umeongea vizuri ila umeharibu kumtaja huyo swetani kwenye hitimisho
 
Unadhalilisha wasukuma bloo,tanzania toka lini ikawa na shida ya maji
 
Katika nchi yenye tatizo la zahanati unaruhusuje watu kuendelea kuzaliana?
Katika nchi yenye tatizo la umeme unaruhusuje viwanda?
Katika nchi yenye tatizo la ajira na madarasa unaruhusuje wanafunzi kufaulu?
Ahsante sana,,

Katika nchi yenye barabara mbovu mbovu unaruhusu je watu kuendelea kununua magari,

Katika nchi yenye ukosefu wa ajira, unakubalije watu kuendelea kusoma na hamna ajira,
 
Ninachojua viroba vilipigwa marufuku siku nyingi mwenzetu wewe unapata wapi au ulikua na stock kubwa sana?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ujamaa ni mfumo wa kijinga Sana kuwahi kutokea hapa Ulimwenguni maana hufanya watu kuwaza mawazo ya kimasikini Sana Kama mleta mada
Mkuu moja ya tusi kubwa unaloweza kunitukana ni kuniita mjamaa. Nauchukia mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…